Katika mchezo huo wa ligi kuu ya vodacom uliochezwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam ulishuhudia mchezo huo ukimaliza dakika 45 za mwanzo bila goli lolote kupatikana

Katika kipindi cha kwanza Yanga SC ndio waliokuwa wanaonekana hatari zaidi huku Mtibwa sugar mashauti yao mengi yakipaa juu ya lango ama kutoka nnje. Wakati yanga SC wakitawala mchezo.
Katika kipindi cha pili Yanga SC walikianza kwa kasi na katika dakika ya 47 walipata faulo ambayo ilipigwa na Haruna Niyonzima ambapo alimtengea Saimon Msuva na Msuva bila ajizi aliachia shuti kali la umbali wa mita 25 na kuinadika Yanga SC goli la kuongoza.
Kuingia kwa goli hilo kuliwaamsha Mtibwa sugar na kupeleka kuanza kupeleka mashambulizi ya ambayo yaliishia kwa walinzi wa yanga SC.
Yanga SC walipoteza nafasi kadhaa za kuongeza ukubwa wa ushinndi wao kupitia kwa Ngoma, Msuva na kuplekea mchezo kumalizika kwa Yanga kuibuka na ushindi wa goli 1-0.
Ushindi huo wa leo unaifanya yanga kufikisha pointi 59 zinazowafanya wakae kilelni wakifuatiwea na Simba SC waneye pointi 57 na Azam FC wenye pointi 55.
Kikosi cha Yanga SC kilikuwa: Deogratius Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, Oscar Joshua, Kevin Yondan/Malimi Busungu dk46, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Vincent Bossou, Simon Msuva, Thabani Kamusoko, Donald Ngoma, Haruna Niyonzima na Deus Kaseke/Amissi Tambwe Dd73.
Mtibwa Sugar: Said Mohamed, Ally Shomari, Majaliwa Shaaban, Andrew Vincent, Salim Mbonde/Boniface Maganga dk83, Shaaban Nditi, Shiza Kichuya/Vincent Barnabas Dd73, Muzamil Yassin, Ibrahim Rajab ‘Jeba’/Henry Joseph Shindika dk52, Suleiman Rajab na Kelvin Friday.

Wakati Coastal union wakiongeza siku za kupambana kubaki ligi kuu ya vodacom, Kagera sugar taratibu inafufua matumani yta timu za chini kubakia ligi kuu kama watapambana mpaka mwisho.
Hii leo katika michezo ya ligi kuu Kagera Sugar iliyopo katika nafasi ya 12 wakiwa na pointi 25 wamepoteza mchezo wao dhidi ya Ndanda FC na kupeleka tofauti ya pointi baina yake na timu ya mwisho kuwa ni pointi 3 baada ya timu ya mwisho Coastal union kushinda.
Kagera sugar hii leo walikuwa katika uwanja wa Nangawanda Sijaona kuwakabili Ndanda FC na dakika 90 zikimalizika kwa NDanda FC kuibukan au shindi wa goli 2-0.
Magoli ya Ndanda FC katika mchezo wa leo yalifungwa kipindi cha pili kupitia kwa Atupele Green na kuifanya NDanda FC kufikisha pointi 33.
Katika mchezo mwingine uliochezwa katika uwanja wa Mkwakwani Coastasl union wameifunga goli 1-0, JKT Ruvu.
Goli la Coastal union hii leo lilifungwa na Geofrey Wambura katika dakika ya 22 na kuifanya Coastal kufikisha pointi 22 wakiwa katika nafasi za chini.
MATOKEO YA MICHEZO YA LEO
YANGA SC 1-0 MTIBWA SUGARNDANDA FC 2-0 KAGERA SUGAR
COASTAL UNION 1-0 JKT RUVU
Msimamo wa Ligi Kuu Msimu Huu
Rn | Timu | P | W | D | L | F | A | Gd | Pts |
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
1 | YANGA | 24 | 18 | 5 | 1 | 57 | 13 | 44 | 59 |
2 | SIMBA SC | 24 | 18 | 3 | 3 | 43 | 13 | 30 | 57 |
3 | Azam FC | 24 | 16 | 7 | 1 | 41 | 16 | 25 | 55 |
4 | MTIBWA SUGAR | 26 | 12 | 7 | 7 | 29 | 19 | 10 | 43 |
5 | T. PRISONS | 26 | 10 | 11 | 5 | 23 | 21 | 2 | 41 |
6 | MWADUI FC | 26 | 9 | 7 | 10 | 25 | 25 | 0 | 34 |
7 | STAND UNITED | 25 | 10 | 4 | 11 | 22 | 22 | 0 | 34 |
8 | NDANDA FC | 27 | 7 | 12 | 8 | 26 | 27 | -1 | 33 |
9 | MAJIMAJI FC | 26 | 9 | 6 | 11 | 20 | 34 | -14 | 33 |
10 | MBEYA CITY | 26 | 8 | 6 | 12 | 28 | 33 | -5 | 30 |
11 | TOTO AFRICANS | 26 | 6 | 9 | 11 | 24 | 36 | -12 | 27 |
12 | KAGERA SUGAR | 27 | 6 | 7 | 14 | 19 | 31 | -12 | 25 |
13 | JKT RUVU | 25 | 6 | 6 | 13 | 24 | 34 | -10 | 24 |
14 | MGAMBO SHOOTING | 26 | 5 | 8 | 13 | 20 | 32 | -12 | 23 |
15 | AFRICAN SPORT | 27 | 6 | 5 | 16 | 11 | 30 | -19 | 23 |
16 | Coastal Union | 27 | 5 | 7 | 15 | 16 | 37 | -21 | 22 |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni