Pambano la marudiano kati ya Al Ahly ya Misri na Yanga litachezwa kwenye uwanja wa Borg Al-Arab wenye uwezo wa kubeba watazamaji 86,000 lakini Chama cha Kandanda nchini Misri kimesema ni mashabiki wasiozidi 15,000 watapewa tiketi za kuingia uwanjani kutazama mchezo huo.
Mkurugenzi mtendaji wa Chama cha Kandanda cha Misri ( EFA), Tharwat Swilan amethibitisha tiketi za mchezo huo hazitauzwa kwa mashabiki kwa njia ya kawaida.
Mashabiki watajaza fomu za maombi ya tiketi mtandaoni kisha bahati nasibu kuchezeshwa kwa ajili ya kuchagua mashabiki watakaotumiwa mualiko wa kuingia uwanjani.
Yanga itakuwa mgeni wa Al Ahly katika mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika utakaochezwa siku ya Jumatano.
Wawakilishi wa Tanzania wanahitaji ushindi wa aina yoyote au sare ya kuanzia mabao 2 ili kuweza kusonga mbele na kufuzu kwa hatua ya makundi kwa mara ya pili.
source: soka360
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni