STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumamosi, 9 Aprili 2016

KIKOSI CHA YANGA DHIDI YA AL AHLY...........


Kikosi cha Yanga kilichoanza dhidi ya Azam FC
Kikosi cha Yanga kilichoanza dhidi ya Azam FC kwenye mchezo wa VPL
Yanga imemaliza maandalizi yao na jana ilirejea jijini Dar es Salaam ikitokea Pemba lakini kocha wao mkuu Hans Pluijm ametamka kwamba kila kitu kwao kipo sawa ingawa mechi ni kitu tofauti.

Pluijm amesema wamefanya maandalizi ya kila aina katika kujiandaa kuwavaa Al Ahly ikiwa ni pamoja na kuwasoma katika mechi zao mbili walizocheza dhidi ya Recreativo Libolo ya Angola ambapo sasa wachezaji wake wanatakiwa kwenda kuyafanya kazi uwanjani aliyowaelekeza.

Amesema Al Ahly ni timu nzuri yenye safu ya ushambuliaji yenye kasi ambapo mabeki wake wanatakiwa kuhakikisha hawaruhusu makosa kufanyika huku pia wakitakiwa kutumia vyema nafasi zao uwanjani.

“Hii ni mechi ngumu tunacheza dhidi ya timu tunahitaji kuwaheshimu lakini sio kuwaogopa, tumefanya maandalizi lakini hii ni hatua moja mechi ni kitu tofauti na mazoezi, nafurahi kuona morali iko juu kwa vijana wangu sasa ni wakati wa kutafsiri tuliyoelekezana mazoezini kuja uwanjani,” amesema Pluijm.

“Kikosi kipo imara ni watu wawili tutakaowakosa ukiacha Haruna (Niyonzima) ambao ni Mbuyu (Twite) mwenye maralia na Matheo (Simon) aliyepata maumivu ya mguu wake wengine wote wako salama.”

Kikosi kitakachoanza kwenye mchezo dhidi ya Al Ahly mechi itakayochezwa kwenye uwanja wa taifa kimepangwa kama ifuatavyo;

Ally MustafaBarthez’, Juma Abdul, Mwinyi Haji,Vicent Bossou, Kelvin Yondani, Thabani Kamusoko, Salum Telela, Simon Msuva, Deus Kaseke, Donald Ngoma na Amissi Tambwe.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox