STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumatatu, 11 Aprili 2016

MNYAMA UAWAWA TAIFA, APIGWA 2-1 NA COASTAL, DROO YA NUSU FAINALI ASFC KUFANYIKA KESHO LIVE

http://cdn5.img.sputniknews.com/images/102507/94/1025079446.jpgBaada ya kutibua rikodi za kutopoteza mchezo kwa Yanga SC na Azam FC, Coastal union leo wamezima ndoto ya Simba SC kuiwakilisha Tanzania Bara katika michuano ya Kombe la shirikisho Afrika Mwakani, baada ya kuwafunga goli 2-1.

Matumaini ya Simba SC kushiriki michuano ya kimataifa mwakani yamebakia katika mbio za ubingwa wa ligi kuu, ambapo anafukuzana kwa karibu na Azam FC na Yanga.

Katika mchezo wa leo wa kombe la TFF uliochezwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam Coastal union walikuwa wa mwanzo kupata goli kupiti kwa Yousuf Sabo kwa mpira wa adhabu aliopiga moja kwa moja na kuiandika Coastal goli la uongozi katika dakika ya 20.

Kuingia kwa goli hilo Simba SC walijaribu kufika langoni mwa Coastal union bila mafanikio yoyote katika kipindi cha kwanza na kuplekea dakika 45 za kwanza kumalizika kwa Coastal union kuibuka na ushindi wa goli 1-0.

Kipindi cha Simba SC walianza kwa mabadiliko ambapo aliingi Hamisi Kiiza na Awadh Juma kuchukuwa nafasi ya Said NDemla na Justice Majabvi .

Mabadiliko hayo yaliongeza kasi kwa Simba SC na katika dakika ya 49 Hamiisi Kiiza aliitendea vyema krosi ya Ibrahim Ajibu na kuiandikia Simba SC goli la kusawazisha.

Kuingia kwa goli ilo kulipeleka kocha Ally Jangalu kumuinua kwenye benchi Ahmad Ally Shiboli na kuingia uwanjani.

Simba SC waliendelea kushambulia kwa kasi huku Coastal union wakitumia mipira ya kushtukiza kupitia kwa Shiboli na Mahadhi.

Katika dakika ya 84 Shiboli akiwa anaenda kumsalimu kipa wa Simba SC beki wa Simba SC Novaty Lufungo alimfanyia madhambi na mwamuzi wa mchezo huo kuamuru penati ipigwe kuelekea langoni mwa Simba SC, huku Lufungo akizawadiwa kadi nyekundu.

Sabo aliifunga penati hiyo kwa ustadi mkubwa na kuiandika Coastal union goli la pili na kupelekea Simba SC kukubali kichapo cha goli 2-1 toka kwa Coastal union.

Bingwa wa michuano hii ndio atakae iwakilisha Tanzania bara katika michuano ya kombe la shirikisho la soka Africa (CAF confederation cup) mwakani.

Droo ya Nusu Fainali inatarajiwa kufanyika kesho Saa 3:00 usiku moja kwa moja kupitia chaneli ya Azam Two ya Azam TV.
 
Robo nyingine za michuano hiyo iliyoanza mwishoni mwa mwaka jana kwa kushirikisha timu 64, Azam FC iliitoa Prisons kwa kuifunga 3-1, Mwadui FC iliitoa Geita Gold kwa kufunga 3-0 na Yanga SC iliwafunga Ndanda FC 2-1.

 
Ikumbukwe bingwa wa Kombe la ASFC ataiwakilisha Tanzania kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika mwakani.

 
Kikosi cha Simba kilikuwa; Vincent Angban, Emery Nimubona, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Hassan Isihaka, Novaty  Lufungo, Justice Majabvi/Hamisi Kiiza dk47, Hassan Kessy, Jonas Mkude, Danny Lyanga, Ibrahim Hajibu na Said Ndemla/Awadh juma dk46.

 
Coastal Union; Fikirini Bakari, Said Jeilan/Ally Ahmed ‘Shiboli’ dk46, Mbwana Hamisi ‘Kibacha’, Abdulhahlim Humud, Twaha Ibrahim ‘Messi’, Godfrey Wambura, Juma Mahadhi na Tumaini Mosha. 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox