STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumamosi, 9 Aprili 2016

YANGA YAWAVIMBIA WAARABU, WATOKA SARE 1-1, NGOMA BADO MBICHI

Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya vodacom Yanga SC wametoka sare na Al-ahly ya Misri katika mchezo wa klabu bingwa Afrika uliochezwa katika uwanja wa Taifa hii leo.

Katika mchezo huo wa kwanza wa mzunguko wa pili wa klabu bingwa Afrika, Yanga SC walianza mchezo kwa kasi na katika dakika ya kwanza walifanikiwa kupata kona ambayo haikuzaa matunda yoyote kwa yanga sc.

Al-ahly wakicheza soka la taratibu na pasi fupi fupi walikuwa wa mwanzo kupata goli kupitia kwa Amri Gamal katika dakika ya 11 ya mchezo
Kuingia kwa goli hilo yanga sc waliendelea kutumia mipira mirefu, kusaka goli la kusawazisha, huku Al-ahly wakipoza mchezo huo.

Yanga walisawazisha goli hilo katika dakika ya 19 baada ya mlinzi wa Al-ahly, Ahmed Sayed kujifunga katika harakati ya kuokoa krosi ya Boubacry na kupeleka dakika 45 za mwanzo kumalizika kwa sare ya goli 1-1.

Katika kipindi cha pili Al-ahly walianza kwa kutawala mpira na katika dakika ya 48 amanusura waandike goli la pili kufuatia shuti la mshambuliaji wa Al-ahly kugonga mwamba.

Kocha wa yanga Pluijim alimpumzisha Deusi Kaseke na nafasi yake kuchukuliwa na Geofrey Mwashuiya, huku akimtoa Amisi Tambwe na kuingia Saimon Msuva kitendo kilichopelekea Yanga kurejesha utawala wake wa mchezo.

Katika dakika ya 78  kipa wa yanga Ally Mustapha Bathezi aliumia na nkukimbizwa hospitali, na nafsi yake kuchukuliwa na Deogratius Munish 'Dida' na mpaka dakika 90 zinakamilika Yanga SC 1-1 Al-ahly.

Kwa matokeo, Yanga italazimika kwenda kushinda ugenini ili kutimiza ndoto za kucheza hatua ya makundi ya michuano hiyo kwa mara ya pili katika historia yao baada ya mwaka 1998.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox