Mechi ya Ligi Kuu ya
Vodacom Tanzania Bara kati ya Ndanda FC ya Mtwara na Young Africans
umerudishwa nyuma kwa siku moja na sasa itachezwa Mei 14, 2016 badala ya
Mei 15, 2016 kama ratiba ya awali inavyosomeka.
Taarifa ya Bodi ya Ligi
Kuu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imesema sababu za kurudisha
nyuma mchezo huo Na. 218 utakaofanyika Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini
Mtwara ni kuipa timu ya Young Africans nafasi ya kujiandaa na kusafiri
kwenda nchini Angola kwenye mchezo wa kimataifa wa Kombe la Shirikisho
Barani Afrika.
Mbali ya mechi hiyo, kuna michezo miwili ambayo
imesogezwa mbele kwa siku moja.
Mechi hizo ni kati ya Simba na Mwadui
ambayo sasa itachezwa Mei 8, 2016 badala ya Mei 7, 2016.
Sababu za
mchezo huo kusogezwa mbele ni kwamba Mei 7, 2016 kutakuwa na mchezo wa
kimataifa utakaozikutanisha Young Africans dhidi ya Esperanca ya Angola
kuwania Kombe la Shirikisho.
Mchezo mwingine uliosogezwa mbele ni kati
ya Kagera Sugar dhidi ya Azam FC ambao sasa utafanyika Mei 8, 2016
badala ya Mei 7, 2016. Sababu za mchezo huo kusogezwa mbele ni Uwanja wa
Kambarage Shinyanga.
Mei 7, 2016 uwanja huo utakuwa na mchezo kati ya
Stand United ya Shinyanga dhidi ya Coastal Union ya Tanga.
Kadhalika
Ligi Kuu Tanzania Bara, inatarajiwa kuendelea kesho Mei 3, 2016 kwa
mchezo mmoja ambao Young Africans ya Dar es Salaam itakuwa mgeni wa
Stand United kwenye Uwanja wa Kambarage, Shinyanga.
Jumatano Mei 4, 2016
Azam FC ya Dar es Salaam itakuwa mwenyeji wa JKT Ruvu ya Pwani kwenye
Uwanja wa Azam, Chamazi nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
Michezo
hiyo itaanza saa 10.000 jioni na kurushwa moja kwa moja na vituo vya
televisheni ya Azam.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni