STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumatatu, 18 Julai 2016

BREAKING NEWZ, RATIBA VPL IMEVUJA, SIMBA GEMU 6 ZA MWANZO TAIFA, YANGA YAANZA NA KIPORO

MABINGWA wa mataji yote nchini, Yanga SC watamenyana na washindi wa pili wa mashindano yote, Azam FC katika mchezo wa Ngao ya Jamii Agosti 17, mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa ratiba ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara iliyovuja Yanga watafungua dimba na JKT Ruvu Agosti 31 Uwanja wa Taifa.

Kwa ujumla Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu wa 2016/ 2017 itaanza Agosti 20, Simba SC wakifungua dimba na Ndanda FC Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, huku Azam wakiikaribisha African Lyon Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.

Mechi nyingine za ufunguzi zitakuwa kati ya Kagera Sugar na Mbeya City Uwanja wa Kaitaba, Bukoba, Toto Africans na Mwadui FC Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza, Stand United na Mbao FC Uwanja wa Kambarage, Shinyanga, Mtibwa Sugar na Ruvu Shooting Uwanja wa Manungu, Turiani, Morogoro na Majimaji na Prisons Uwanja wa Majimaji Songea.  


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox