STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumatatu, 18 Julai 2016

YANGA HUU SI MWISHO WENU,CHUKULIENI KAMA CHANGAMOTO..........



KWA hesabu za harakaharaka, timu ya Yanga imeshatupwa nje ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kucheza mechi tatu na kufungwa mbili huku ikiambulia sare moja.



Kwenye kundi lake, yenyewe ndiyo inaburuza mkia ikiwa na pointi moja iliyoipata juzi Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa, Dar ilipofungana bao 1-1 na Medeama na kumaliza mzunguko wa kwanza.



Katika mzunguko huo wa kwanza, Yanga imecheza mechi mbili nyumbani dhidi ya TP Mazembe na Medeama huku moja ikiwa ni ya ugenini ambayo ni dhidi ya MO Bejaia.

Mzunguko wa pili watacheza mbili ugenini dhidi ya Medeama na TP Mazembe kabla ya kuwakaribisha MO Bejaia hapa nyumbani.




Kama Yanga inataka kufuzu hatua ya nusu fainali, inahitaji kufanya maombi ili wapinzani wake wateleze kwenye mechi zijazo huku yenyewe ikusanye pointi zote tisa katika mechi zake hizo tatu na kumaliza na pointi kumi.

Kwenye soka lolote linaweza kutokea lakini kiuhalisia inaonekana ni ngumu kwa Yanga kutoka mkiani na kutinga nusu fainali ambapo timu mbili kutoka kila kundi ndizo zitafuzu.

 IMG_5687_20160716201256602_20160716201418797

Ukiangalia kwenye michezo yake ya nyuma, Yanga haikuwa ikifanya vizuri ugenini zaidi ya kuutumia uwanja wake wa nyumbani ambapo sasa hivi watacheza hapo mechi moja tu kati ya tatu zilizosalia.

Licha ya kuonekana kuwa na ugumu, lakini binafsi nawapongeza kwa kufika hapo kwani kwao ni mafanikio makubwa kutokana na muda mrefu kuishia hatua za mwanzoni.

Kilichobaki sasa ni kutokata tamaa kwa sababu ukiangalia ukanda mzima wa Afrika Mashariki, hakuna timu iliyobaki katika michuano ya kimataifa kwa ngazi ya klabu zaidi ya Yanga.
Yanga iliyoanza msimu huu kwa kuiwakilisha Tanzania kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika kabla ya kudondokea Kombe la Shirikisho, msimu ujao tena itashiriki Ligi ya Mabingwa kutokana na kuwa mabingwa wa Ligi Kuu Bara msimu uliomalizika Mei, mwaka huu.


Hii ni nafasi nyingine kwao kusahihisha makosa yaliyotokea msimu huu na nadhani kama kweli watakuwa na nia thabiti bila shaka watafanikiwa.




Kuna msemo unasema kuteleza si kuanguka, Yanga inatakiwa kujifunza kwa kile walichokiona msimu huu ili msimu ujao wafikie malengo yao japo nusu yake endapo watashindwa yote.

Yanga wanatakiwa kufahamu kuwa hakuna timu iliyofanikiwa kimataifa au ngazi yoyote ile bila ya kupitia misukosuko, hata hizo zinazotesa leo nazo zilikuwa na wakati mgumu huko nyuma au zingine hata sasa zinakumbana na matatizo licha ya kuwa na mafanikio.

Licha ya hivyo, najua wapo waliofurahia kufanya vibaya kwa Yanga kutokana na itikadi zao kiushabiki, hawapaswi kubadili mawazo yao na waendelee kufurahi ili Yanga waumie na mwisho wake watafute njia za kuwabadilishia kibao.


Group A

Pos Team
Pld W D L GF GA GD Pts





1 Democratic Republic of the Congo TP Mazembe 3 2 1 0 4 1 +3 7





2 Algeria MO Béjaïa 3 1 2 0 1 0 +1 5




3 Ghana Medeama 3 0 2 1 2 4 −2 2





4 Tanzania Young Africans 3 0 1 2 1 3 −2 1





mdosejr@gmail.com

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox