STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumatano, 20 Julai 2016

HANS VAN DER PLUIJM AMEFANYA MAAMUZI HAYA KUHUSU HATMA YAKE KLABUNI YANGA.............

 


MHOLANZI, Hans van der Pluijm amesaini Mkataba mpya wa miaka miwili kuendelea kufundisha klabu ya Yanga ya Dar es Salaam.

   
Pluijm amesaini Mkataba huo jana makao makuu ya klabu, Jangwani, Dar es Salaama baada ya kazi nzuri msimu uliopita, akiipa timu mataji yote matatu ya nyumbani.
  Pluijm aliiwezesha Yanga kuwapiku wapinzani wao wakubwa, Azam FC katika mbio za mataji ya Ngao ya Jamii, Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara na Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Kombe la Azam Sports Federation Cup (ASFC).

 
Pluijm akisaini Mkataba mpya wa kuendelea kufundisha Yanga SC jana

Na pia akaiwezesha timu hiyo kukata tiketi ya kucheza hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kuitoa Sagrada Esperanca ya Angola.


Yanga iliangukia kwenye kapu la kuwania kucheza hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho baada ya kutolewa na Al Ahly ya Misri katika hatua ya 16 Bora ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

 
Na pamoja na kucheza mechi tatu za Kundi A Kombe la Shirikisho bila ushindi, wakifungwa 1-0 na TP Mazembe, sare ya 1-1 na Medeama zote nyumbani Dar es Salaam na kufungwa 1-0 na MO Bejaia Algeria, lakini Pluijm amepewa Mkataba mpya.  

 
Ikumbukwe, Pluijm yupo katika kipindi cha pili kufundisha Yanga baada ya awali kufundisha kwa nusu msimu mwaka 2014, akimpokea Mholanzi mwenzake, Ernir Brandts.

 
Alikwenda Al Shoalah FC ya Saudi ya Arabia na nafasi yake ikachukuliwa na Mbrazil, Marcio Maximo ambaye naye alifanya kazi kwa nusu msimu kabla ya Pluijm kurejeshwa Januari mwaka jana. 

 
Saudi Arabia ambako alikwenda na aliyekuwa Msaidizi wake, Yanga SC, Charles Boniface Mkwasa – Pluijm  aliondoka baada ya kutofautiana na uongozi wa timu uliotaka kumsajilia wachezaji asiowataka.

 
Franciscus Johannes ‘Hans’ van der Pluijm alizaliwa Januari 3 mwaka 1949 na alianzia kwenye kucheza soka akiwa kipa.

 
Enzi zake aliidakia kwa miaka 28 klabu ya FC Den Bosch akicheza mechi 338 ndani ya misimu 18 na alipostaafu baada ya kuumia goti akawa kocha wa timu hiyo.


Katibu Mkuu wa Yanga, Baraka Deusdedit akimshuhidia Pluijm anavyotia dole gumba kwenye fomu za Mkataba mpya
Alianza vyema ukocha akiiwezesha FC Den Bosch kutwaa ubingwa wa Daraja la Kwanza na kupanda Ligi Kuu na ndiye aliyempa nafasi ya kwanza mshambuliaji Ruud van Nistelrooy akiwa kinda wa miaka 17 tu kucheza kikosi cha kwanza cha timu hiyo.
 
Aprili mwaka 1995, alisaini Mkataba wa miaka miwili na SBV Excelsior kabla ya kutimuliwa Januari 1997 na nafasi yake ikachukuliwa na Msaidizi wake, John Metgod. 

 
Hiyo ilifuatia timu hiyo ya Rotterdam kushinda mechi mbili tu na sare tatu katika mechi 17 za msimu mzima.

 
Baada ya kuboronga Ulaya, ndipo akahamia Afrika mwaka 1999, alipokwenda kufundisha Ashanti Gold SC ya Ghana, akianza na Mkataba wa mwaka mmoja. 

 
Ajax ya Uholanzi ikanunua hisa katika klabu hiyo Ijumaa ya Juni 18, mwaka 1999 asilimia 51 naye akatupiwa virago na kuhamia Saint-George SA ya Ethiopia kabla ya mwaka 2010 kujiunga na B-juniors Feyenoord ya Ghana, ambayo ni tawi la timu hiyo ya Rotterdam.

 
Mwaka 2012 alijiunga na Berekum Chelsea ambako pia alifukuzwa mwaka jana na kuhamia Medeama ya Ghana pia ambako nako alifukuzwa baada ya mechi saba tu, kufuatia matokeo mabaya mwanzo mwa msimu, akivuna pointi nane kati ya 21.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox