STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Alhamisi, 21 Julai 2016

HUYU MBUYU TWITE HAFAI HATA KIDOGO AISEE...!


 

KIRAKA wa Yanga, Mnyarwanda mwenye asili ya DR Congo, Mbuyu Twite, ndiye mchezaji aliyeweka rekodi ya kipekee kwenye kikosi hicho mpaka sasa katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika hatua ya makundi.

 


Rekodi hiyo ni ile ya kucheza nafasi tatu tofauti katika mechi tatu mfululizo za michuano hiyo ambayo Yanga imecheza mpaka sasa.

Twite ambaye kuihalisia ni kiungo mkabaji, amekuwa akichezeshwa nafasi tofauti uwanjani na mara kadhaa huonyesha kiwango cha hali ya juu bila ya kumuangusha kocha wake, Mholanzi, Hans van Pluijm pamoja na benchi zima la ufundi la timu hiyo.

Kiungo huyo hivi karibuni alikuwa kwenye hatari ya jina lake kukatwa kikosini hapo baada ya mkataba wake kumalizika, lakini mabosi wake wakajiuliza mara mbili na kumpa mkataba mpya wa miaka miwili ambapo kwa sasa wanaona uamuzi wao wa kumbakisha unaleta majibu chanya.

Nimemfuatilia kwa umakini mchezaji huyo katika mechi hizo tatu na kubaini amecheza zote ambazo ni jumla ya dakika 270.

                            MO Bejaia vs Yanga

 


Katika mchezo huu wa kwanza wa makundi uliopigwa Juni 19, mwaka huu huko nchini Algeria, ulimalizika kwa Yanga kufungwa bao 1-0.

Kwenye mchezo huu Twite alicheza beki wa kulia baada ya Juma Abdul kuwa majeruhi huku mchezaji mpya kikosini hapo, Hassan Kessy akizuiliwa kucheza kutokana na uhamisho wake kutoka Simba kuonekana haujakamilika.

Kwa dakika zote tisini za mchezo huo, Twite alicheza vizuri japo siyo sana, lakini pia bao walilofungwa lilitokea upande wake ambapo alichelewa kukaba, ikapigwa krosi iliyomkuta mfungaji, Yassin Sahli.


                              
                           Yanga vs TP Mazembe


Huu ulikuwa mchezo wa pili wa hatua hiyo. Yanga ilikuwa nyumbani kwenye Uwanja wa Taifa, Dar, mchezo huo ulimalizika kwa Yanga kufungwa tena bao 1-0.

Kutokana na mabeki wa kushoto wa Yanga, Oscar Joshua kuwa majeruhi huku Haji Mwinyi akitumikia adhabu ya kadi nyekundu aliyoipata walipocheza na MO Bejaia, Twite akachukua mikoba yao na kucheza kwa dakika zote tisini. 

Jumla akawa amecheza dakika 180 katika nafasi za beki wa kulia na kushoto.

Kwa kiasi kikubwa alifanikiwa kuwadhibiti washambuliaji wa TP Mazembe ambapo baada ya kuona hapitiki kirahisi, wakabadilisha njia ya kuipenya ngome ya Yanga.

                            Yanga vs Medeama 
 


Mzunguko wa kwanza wa hatua ya makundi ukamalizika kwa Yanga kutoka sare ya bao 1-1, mchezo uliopigwa Uwanja wa Taifa, Dar.

Katika mchezo huu, Pluijm akamchezesha Twite kama kiungo mkabaji (namba sita) huku Mzimbabwe, Thabani Kamusoko akicheza kiungo wa juu yaani mchezeshaji (namba nane).

Twite alicheza nafasi hiyo kwa dakika 78, kabla ya kupelekwa beki ya kushoto baada ya Oscar Joshua aliyekuwa akicheza upande huo kufanyiwa mabadiliko na kuingia Mnyarwanda, Haruna Niyonzima aliyeenda kucheza kiungo mchezeshaji na Kamusoko kurudi kukaba chini.

Katika nafasi ya kiungo, Twite alicheza vizuri kwa kushirikiana na Kamusoko, lakini alionekana kupungua kasi kidogo alipopelekwa pembeni.

Katika nafasi hizo zote, imebainika kuwa licha ya kuzimudu, lakini anacheza vizuri zaidi kiungo mkabaji huku zile zingine akisuasua kwa namna moja ama nyingine.

mdosejr@gmail.com

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox