STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Alhamisi, 14 Julai 2016

TANZANIA YAPAA VIWANGO VYA FIFA KWA NAFASI 13...........


TANZANIA imekwea kwa nafasi 13 mpaka kufikia nafasi ya 123 katika viwango vya ubora vipya vilivyotolewa na Shirikisho la Soka Duniani-FIFA leo. 
 http://api.ning.com/files/dj7KjSQgc-RzBtAZHNJs8lU06gKsoJHoDUkx2-zIs4y9qOvdDTPr0xpgFdIKSDR4AuMARcArGhcNRGx2vlKb0m2aOd3cZtoK/taifastarz.jpg
Mwezi uliopita Tanzania ilikuwa katika nafasi ya 136 lakini mwezi huu imepanda na kushinda nafasi hiyo huku kwa upande wa Afrika ikishika nafasi ya 36 ikizizidi nchi za Burundi iliyopo nafasi ya 125 duniani na 38 Afrika na Sudan Kusini nafasi ya 153 kwa 47 kwa nchi ukanda wa Afrika Mashariki. 
 
Nchi inayoongoza kwa ukanda wa Afrika Mashariki ni Uganda waliopo nafasi ya 69 duniani na 15 Afrika wakifuatiwa na Kenya waliopo nafasi ya 86 duniani na 22 Afrika na Rwanda ndio wanaoshika nafasi ya tatu wakiwa katika nafasi ya 111 duniani na 32 Afrika. 
 
Kwa upande wa Afrika orodha hiyo bado imeendelea kushikiliwa na Algeria ambao wako nafasi ya 32 duniani wakifuatiwa na Ivory Coast katika nafasi ya 35, Ghana nafasi ya 36, Senegal nafasi ya 41 na Misri ndio anakamilisha tano bora ya Afrika wakiwa nafasi ya 43. 
 
Kwa upande wa orodha za jumla, Argentina bado wameendelea kukaa kileleni wakifuatiwa na Ubelgiji katika nafasi ya pili, Colombia nafasi ya tatu, Ujerumani nafasi ya nne, mabingwa wa Copa America Chile nafasi ya tano na mabingwa wa Ulaya Ureno wao wako nafasi ya sita.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox