STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumamosi, 16 Julai 2016

YANGA GEMU 3 POINTI 1, LOLOTE LINAWEZA KUTOKEA, YABURUZA MKIA

Mabingwa wa ligi kuu ya Tanzania Bara Yanga SC wameeendelea kujiweka katika  wakati mgumu wa kutinga hatua ya nusu fainali ya kombe la shirikisho Afrika (CAF Confederation Cup) baada ya kulazimishwa sare ya goli 1-1 na Medeam FC ya nchini Ghana.
image Katika mchezo huo uliochezwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, Yanga SC waliuwanza mchezo kwa kasi na katika dakika ya pili ya mchezo waliandika goli la kuongoza kupitia kwa Donald Ngoma akimalizia pasi safi ya Thaban Kamusoko.
Kabla ya goli hilo kuingia Yanga SC walipoteza nafasi ya kufunga goli la mapema baada ya jitihada ya kipa wa Medeama na safu yake ya ulinzi kuokoa hatari hiyo, na yanga kutengenza shambulia jingine liliozaa goli hilo la Ngoma.

Kuingia kwa goli hilo kuliwafanya Medeama kucheza kwa tahadhari kubwa na huku wakimuweka mchezaji mmoja mbele.
Katika dakika ya17 Medeama walifanikiwa kupata goli la kuswazisha kufuatia mpira wa kona uliochezwa na wachezaji wa tatu wa Medeama na kufunga goli hilo kupitia kwa Bernard Danso.
Kuingia kwa gol hilo kuliongeza kasi ya mchezo huku yanga sc wakiendelea upoteza nafasi, wakati Medeam muda mwingi wakiwa nyuma huku wakitumia mipira mirefu katika mashambulizi ya kushtukiza.
Kipindi ha pili hali iliendelea kwa hivyo kwa yanga kwa kuendelea kupoteza nafasi za kupatia goli huku Medeama wakipoteza nafasi mbili walizofanikiwa kutengeneza.
Nafasi za wazi zaidi walizotengeneza Yanga SC ni kiupitia kwa Obrein Chirwa na Amisi Tambwe ambapo kila mmoja alipata fursa ya kukutana uso kwa uso na kipa Medeama na kushindwa kuvuisha mpira kwa kipa huyo aliyeokoa michomo mingi ya yanga hii leo na kupelekea mchezo kumalizika kwa sare ya goli 1-1.
 
Licha ya mabadiriko yaliyofanywa kwa mpigo na Yanga kwa kumtoa Oscar Joshua nafasi ikichukuliwa na Juma Mahadh, Amisi Tambwe na kuingia Haruna Niyonzima haikusaidi timu hiyo kupata alama 3 japo mpira uliongezeka kasi baada ya mabadiriko hayo

Matokeo hayo ya leo yanifanya yanga kuwa wamwisho katika kundi B wakiwa na pointi 1, wakati Medeam wakiwa na pointi 2 na TP Mazembe wakiwa kileleni kwa pointi 6, wakati Mo bejaina wanaocheza na Mazembe kesho wakiwa wa pili kwa pointi 4.

Kikosi cha Yanga SC kilikuwa; Deogratius Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, Oscar Joshua/Juma Mahadhi, Kelvin Yondani, Mtogo Vincent Bossou, Mbuyu Twite, Thabani Kamusoko, Simon Msuva, Obrey Chirwa, Amissi Tambwe/Haruna Niyonzima dk na Donald Ngoma.
 
Medeama FC; Daniel Adjei, Samuel Adade, Moses Sapong, Paul Adoo/Salufu Moro dk62, Daniel Amouah, Kwesi Donsu, Erick Kwakwa, Kwame Boahene, Abbas Mohamed, Bernard Ofori na Enock Atta Agyei/Malik Akowuah dk79.   

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox