STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Ijumaa, 15 Julai 2016

IBRAHIMOVICH KUWAKOSA MAN CITY, RENATO SANCHEZ KUTAKIWA OLD TRAFFORD,FERGIE AFUNGUKA KUHUSU CR7..

                            

 

 

                                

                   HABARI KUBWA ZA KIMICHEZO BARANI ULAYA

 

                        

 

                      SANCHEZ AMPA WENGER MCHECHETO.

 

KLABU ya Arsenal inahaha kuhakikisha Alexis Sanchez anakuwa fiti kabla ya mechi yao ya ufunguzi ya msimu mpya wa Ligi Kuu baadae mwezi ujao. 

Sanchez alipata majeruhi ya kifundo cha mguu wakati wa michuano ya Copa America na amekuwa akipatiwa matibabu katika kipindi hiki cha mapumziko ya kiangazi. 

Arsenal wamekuwa akifuatilia kwa karibu maendeleo ya nyota wao huyo na kuna hofu anaweza kukosa mwanzo wa msimu ambapo timu hiyo hiyo itaikaribisha Liverpool katika Uwanja wa Emirates Agosti 14 mwaka huu.

 Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger atataka Sanchez awe fiti ka ajili ya mchezo huo haswa kutokana na uhaba wa washambuliaji alionao kutokana na michuano ya Ulaya iliyomalizika hivi karibuni. 

Kutokana na michuano hiyo Olivier Giroud, Mesut Ozil na Aaron Ramsey hawatajiunga na wenzao kwa mazoezi ya maandalizi msimu mpaka Agosti 8 ikiwa ni siku saba kabla ya mchezo dhidi ya Liverpool.


RONALDO NDIO MCHEZAJI BORA KUWAHI KUTOKEA KWA KIZAZI HIKI - FERGUSON.

MENEJA wa zamani wa Manchester United, Sir Alex Ferguson anaamini hamu ya soka aliyonayo Cristiano Ronaldo inamtenganisha na wote akiwa kama mchezaji bora duniani kwasasa. 

Baada ya kuiongoza Real Madrid kutwaa taji lake la pili la Ligi ya Mabingwa Ulaya katika kipindi cha miaka mitatu, Ronaldo aliiongoza timu ya taifa ya Ureno kutwaa taji la michuano ya Ulaya kwa kuwafunga wenyeji Ufaransa Juni 10 mwaka huu.

 Ferguson ambaye alikuwepo Stade de France kushuhudia Ronaldo akitwaa taji hilo la Ulaya, hana shaka kuwa juhudi kubwa alizokuwanazo nyota huyo ndio sababu kubwa ya mafanikio aliyonayo sasa. 

Ferguson mwenye umri wa miaka 74, ambaye 
amefanya kazi na Ronaldo kwa miaka sita akiwa na United, amesema uchu na hamu kubwa ya mchezo wa soka aliyonayo Ronaldo ndio inayomfanya kufikia mafanikio hayo hivi sasa.

 Ferguson aliendelea kudai kuwa Ronaldo amekuwa akijituma kila siku na mara zote amekuwa akitaka kuimarika zaidi na kushinda haswa katika mechi kubwa. 

Kocha huyo mkongwe amesema kwa kawaida wachezaji wakubwa hucheza kwa kiwango cha juu kwa miaka mitano au sita tu lakini Ronaldo ni tofauti kwa amefanya hivyo kwa zaidi ya miaka 10 ndio anadhani ndio mchezaji bora kabisa kutokea katika kizazi hiki. 


                      MAN UNITED BADO WAMSARANDIA SANCHEZ.

KLABU ya Manchester United inadaiwa kuwa tayari imeshaiuliza Bayern Munich kuhusu kutenzi cha kutengua mkataba wa Renato Sanchez. 

United walikuwa wakiongoza mbio za kumsajili chipukizi huyo mwenye umri wa miaka 18 mapema mwaka huu lakini walishindwa mbio hizo na Bayern ambao walimsajili kwa kitita cha paundi milioni 37.7 kutoka Benfica. 

Lakini Mourinho na United wameonyesha kufurahishwa na kiwango kikubwa alichoonyesha Sanchez wakati akiitumikia Ureno katika michuano ya Ulaya na sasa wanataka kujulishwa kuhusu kitenzi chake alichowekewa katika mkataba wake na Bayern.

Mourinho ambaye pia anamfukuzia Paul Pogba, inadaiwa ameshangazwa kwa United kuikosa nafasi ya kumsajili Sanchez mpaka akaenda Bayern.

CHELSEA YATENGA PAUNDI MILIONI 80 KUSAJILI WAWILI KA MPIGO.

KLABU ya Chelsea inadaiwa kukaribia kuwasajili nyota wawili N’Golo Kante na Kalidou Koulibaly kwa jumla ya paundi milioni 80. 

Kante ambaye amekuwa mmoja kati ya viungo bora wa Ligi Kuu msimu uliopita wakati Leicester City walitawadhwa mabingwa, anadaiwa kukaribia kutua Stamford Bridge kwa kitita cha paundi milioni 30 kiasi ambacho kimekubaliwa na pande zote mbili. 

Kufuatia kumkosa beki wa kati wa Juventus Leonardo Bonucci, Antonio Conte sasa amegeuzia nguvu zake kwa Koulibali anayayekipiga Napoli, wakati akijaribu kuimarisha safu yake ya ulinzi.

 Mabingwa hao wa Serie A wanadaiwa kutaka paundi milioni 50 kwa nyota huyo mwenye umri wa miaka 25, na pamoja na Everton pia kutajwa kumuwania beki huyo Chelsea wanaamini wao ndio wenye nafasi kuba ya kumnasa.


             MOURINHO KUMUACHA IBRAHIMOVIC ZIARA YA CHINA.

MENEJA mpya wa Manchester United, Jose Mourinho anafikiria kumuacha Zlatan Ibrahimovic wakati watakaposafiri kwa ajili ya ziara ya kwenda kucheza mechi mbili nchini China Jumanne ijayo. 

Nyota wa kimataifa wa Uingereza Wayne Rooney, Chris Smalling na Marcus Rashford wanatarajiwa kuwepo katika ziara hiyo. 

Hata hivyo, Mourinho amesema wachezaji hao hawatacheza mchezo dhidi ya Borussia Dortmund utakaofanyika jijini Shanghai Julai 22 na ule dhidi ya mahasimu wao Manchester City utakaofanyika jijini Beijing Julai 25. 

Ibrahimovic mwenye umri wa miaka 34, yeyey anatarajiwa kutojumuishwa kabisa katika kikosi hicho.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox