STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumatatu, 1 Agosti 2016

MO DEWJI ATOA KAULI WAKATI HUO VIONGOZI WA SIMBA WAMUITA MEZANI.....

 

UONGOZI wa Simba SC umemuita mfanyabishara
Mohamed Gulam Dewji kujadili naye mpango wa kununua hisa za klabu hiyo.

 
Katika barua iliyosainiwa na Katibu Mkuu wa klabu, Patrick Kahemele leo – uongozi wa Simba umemuomba Mo Dewji kuhudhuria kikao cha Kamati ya Utendaji Agosti 15, mwaka huu.


 
 

Na wamepeleka kikao hicho Agosti 15 kwa sababu wiki hii watakuwa wametingwa na shughuli za wiki ya Simba kuelekea tamasha la Simba Day Agosti 8, mwaka huu.
 
Mapema leo, Mo Dewji amesema amewasilisha barua rasmi ya kutaka kuinunua klabu ya Simba ya Dar es Salaam.



Mo Dewji ameitwa kwenye kikao cha Kamati ya Utendaji ya Simba wiki ijayo


































Na hatua hiyo inakuja siku moja baada ya Mkutano Mkuu wa mwaka wa Simba SC jana kuridhia mabadiliko kwa kuingia kwenye mfumo wa kuuza hisa.
 
Mo Dewji, tajiri namba moja kijana Afrika kwa mujibu wa jarida la Forbes la Marekani, ameyasema hayo asubuhi ya leo katika Mkutano na Waandishi wa Habari, jengo la Golden jubilee Towers, Mtaa wa Ohio, Dar es Salaam.  

 
“Leo asubuhi kitu cha kwanza nimefanya ni kuandika barua na kuipeleka ofisini kwa Rais wa Simba, Evans Aveva. Na nimefika nimekuta ofisi yake haijafunguliwa, ikifunguliwa ataikuta barua ya kwanza ni yangu pale,”amesema Mo Dewji.

 
Mo amesema katika barua hiyo ameandika kwamba yeye ni mwanachama aliyewahi kuwa mfadhili wa timu, ambaye sasa anataka awekeze Sh. Bilioni 20 kwa kununua asilimia 51 ya hisa za klabu.

 
“Nimesema fedha hizo zitawekwa kwenye akaunti maalum na hazitaguswa. Nataka mchakato huu utimie ndani ya miezi mitatu kama inawezekana,”amesema. 

 
Hata hivyo, Mo amesema anasikitika baadhi ya viongozi wa Simba chini ya rais Aveva wanaonekana hawataki mabadiliko.
“Jana nilikuwa nafuatilia mkutano, nilisikia hoja kadhaa kwa namna moja au nyingine, ziliniumiza na zilikuwa za upotoshaji. 


Wanasema natangaza kwenye vyombo vya habari tu, hatujawahi kukutana. Leo niwe muwazi zaidi, nimekwishakutana na Aveva zaidi ya mara tatu. Na amewahi kuja ofsni kwangu zaidi ya mara tatu. Alikuja na (Geoffrey Nyange) Kaburu (Makamu wa Rais).  Hizi dhana tunamsikia Mo kwenye vyombo vya habari si za kweli,”. 
 
“Lakini pia, kulikuwa kuna hoja Mo anasema kwa maneno si kwa maandishi, sisi tulikuwa tunangojea wanachama waridhie mabadiliko ya mfumo, kwa kuwa wameridhia na ninawashukuru sana. 

 
Leo asubuhi kitu cha kwanza nimefanya ni kuandika barua na kuipeleka ofisini kwa Rais wa Simba, Evans Aveva,”amesema na kuongeza. “Sasa barua kapata, nitamuomba Evans ajaribu kukaa na Kamati ya Utendaji, ili waone namna ya kufanikisha hili jambo haraka,”aliongeza Dewji.




Aidha, Dewji alisema ahadi yake ya kusaidia usajili wa wachezaji Simba SC wakikubali mabadiliko iko pale pale. “Ahadi yangu iko pale pale, lakini lazima viongozi waridhie,”alisema.
 
Katika Mkutano Mkuu wa mwaka wa Simba SC uliofanyika jana, uongozi uliridhia ombi la wanachama kutaka mabadiliko na kuingia kwenye mchakato huo mara moja.

 
Na wanachama walishinikzia mabadiliko baada ya Mo Dewji kutangaza ofa ya kununua asilimia 51 ya hisa za klabu kwa Sh. Bilioni 20 na kuwekeza.

 
Na Mo ameahidi kuifanya Simba iwe klabu bora zaidi nchini iwapo atafanikiwa kupewa hisa.  



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox