STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumanne, 2 Agosti 2016

BAADA YA KUICHAPA BUKINAFASO, KESHO SIMBA KUCHEZA MECHI YA MWISHO YA KIRAFIKI DHIDI YA...?


Simba ilishinda tena mchezo wake wa kirafiki dhidi ya timu ya Burkina Faso, mchezo huo uliochezwa jana jioni ulimalizika kwa Simba kupata ushindi wa goli 5-0.
 
 

Magoli ya Simba yamefungwa na Ibrahimu Ajibu dakika ya 1 na dakika ya 35, Mussa Ndusha Dakika ya 15′ Shizya Kichuya dakika ya 55 na Said Ndemala dakika ya 65 mchezo huu ni wa tatu kwa timu ya Simba kupata ushindi katika michezo yote mitatu ya kirafiki aliyocheza tangua iweke kambi mkoani Morogoro.


Imeshacheza na Timu ya Polisi Moro wakapata ushindi wa 5-0,Simba vs Moro Kids ikashinda kwa goli 2-0. Simba inatarajia kucheza mchezo mwingine wa kirafiki siku ya Jumatano dhidi ya timu ya Manispaa ya Kinondoni na kujiandaa kurudi Dar kwa ajili ya Simba day August 8.




PICHA MBALIMBALI KATIKA MCHEZO HUO; 
 
                                                               Waamuzi katika mchezo huo
 



                            Kocha wa Bukinafaso Ulimboka Mwakingwe



             Wachezaji wa Simba wakiteta jambo katika mchezo dhidi Bukinafaso


 
Mchambuzi wa michezo na mtangazaji wa Planet Fm 87.9 Morogoro,Mr Choi (kulia) akiteta jambo na msemaji wa 77 United iliyo daraja la pili mara baada ya mchezo wa Bukinafaso na Simba.






Mpiga picha wa gazeti namba moja la michezo Tanzania Championi, Omary Mdose akiwa makini kuchukua matukio ya mchezo kati ya Simba dhidi ya Bukinafaso .
 
             Mchambuzi wa michezo na mtangazaji wa Planet Fm 87.9 Morogoro Mr'Choi (kushoto), akiwa na msemaji wa 77 United Abubakar Mkingie (katikati) pamoja na ripota wa Sports Xtra, Peter Andrew.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox