STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumatano, 3 Agosti 2016

STORI MBILI KUBWA MICHEZONI, MAVUGO KATUA SIMBA, KIPRE TCHETCHE RASMI ASEPA AZAM....

 


                                STORI YA KWANZA;

HATIMAYE baada ya danadana za muda mrefu, mshambuliaji wa kimataifa wa Burundi, Laudit Mavugo amewasili usiku wa Jumatano kujiunga na Simba SC.

 
 






Mavugo aliwasili Saa 4:30 Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam na kupokewa na Makamu wa Rais wa Simba, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ aliyempeleka hotelini kupumzika.

 
Asubuhi ya Alhamisi, Mavugo atakuwa na mazungumzo na uongozi wa Simba SC kabla ya kwenda kambini Chuo cha Biblia mjini Morogoro kujiiunga na wenzake.  























Laudit Mavugo baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam usiku wa Jumatano

 































Na mshambuliaji huyo wa Vital’O ya kwao, anakuja Tanzania baada ya mpango wa kujiunga na klabu ya Tours ya Ligi Daraja la Pili, Ufaransa maarufu kama Ligue 2 kukwama.
 
Mavugo alikwenda Ufaransa wakati tayari Simba SC wamesema wamekwishaingia Mkataba na mchezaji huyo kuanza kuwatumikia kuanzia msimu ujao.



Mavugo (kulia) akiwa na Makamu wa Rais wa Simba, Kaburu baada ya kuwasili JNIA







 



Hapa ni baada ya Mavugo kuwasili kabla ya kuvalishwa jezi ya Simba

 




















































































Wakati huo huo: Simba SC imefungwa 1-0 na KMC ya Kinondoni jioni ya Jumatano katika mchezo wa kirafiki uliofanyika Uwanja wa Highlands, Bigwa mkoani Morogoro.
 
Huo unakuwa mchezo wa kwanza Simba SC kupoteza chini ya kocha mpya, Mcameroon, Joseph Marius Omog baada ya awali kushinda mechi zote tatu, 5-0 dhidi ya Burkina Fasso, 2-0 dhidi ya Moro Kids na 6-0 dhidi ya Polisi Morogoro.






 
 

Katika hatua nyingine, timu ya Interclube ya Angola haitakuja kucheza na Simba katika sherehe za miaka 80 ya klabu hiyo, maarufu kama Simba Day badala yake itakuja AFC Leopards ya Kenya.


                                  STORI YA PILI; 


KIPRE TCHETCHE ASAINI MKATABA OMAN;






Mshambuliaji nyota wa Azam FC, Kipre Tchetche raia wa Ivory Coast ametua rasmi katika kikosi cha Al Nahdha  FC nchini Oman.



Azam FC ilitangaza Tchetche ambaye aligoma kurejea nchini kuwa ina mkataba naye wa mwaka mmoja na hatakwenda popote.




Lakini tayari Tchetche ametambulishwa jijini Muscat kujiunga na Al Nahda moja ya klabu kubwa zinazochipukia nchini humo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox