Vinara
wa ligi kuu ya vodacom Simba SC wameongeza tofauti ya pointi kati yao na
mabingwa watetezi Yanga kutoka pointi moja mpaka pointi 4 baada ya leo kuibuka
na ushindi wa goli 1-0 mbele ya JKT Ruvu mchezo uliochezwa katika uwanja wa
uhuru jijini Dar es salaam.
Katika mchezo huo uliokuwa wa kasi na kushambuliana kwa zamu Simba SC iliwabidi kungoja mpaka dakika ya 45 kuandika goli pekee la mchezo huo lililofungwa na Mzamiru Yassin kunako dk ya 49, aliyemalizia krosi ya Pastori Athanas baada ya kipa wa JKT Ruvu kuanguka chini baada ya kuoka mpira.
Katika kipindi cha pili Simba SC walitengeneza nafasi nyingi ukilinganisha na kipindi cha kwanza lakini safu yake ya ushambuliaji ilishindwa kuzitumia nafasi hizo.
JKT Ruvu nao hawakuwa nyuma katika kutengeneza nafasi, ambazo nao walishindwa kuzitumia na kupeleekea mchezo kumalizika kwa Simba SC kushinda goli 1-0.
Kwa ushindi huo, Simba inafikisha pointi 42 baada ya kucheza mechi 17 huku wakifatiwa na Yanga yenye point 37
JKT Ruvu: Hamis Seif, Salim Gilla,
Michael Aidan, Frank Nchimbi, Yussuf Chuma, Kelvin Nashon, Edward Joseph,
Hassan Dilunga, Hassan Materema, Mussa Juma/Kassim Kisengo dk80 na Ally
Bilal/Atupele Green dk62.
MATOKEO MENGINE KUNAKO VPL
1. Majimaji 1-1 Azam FC
wafungaji katika mchezo huo ni Yahay Muhammed kwa upande wa Azam FC na Kondo Alex kwa upande wa Majimaji.
1. Majimaji 1-1 Azam FC
wafungaji katika mchezo huo ni Yahay Muhammed kwa upande wa Azam FC na Kondo Alex kwa upande wa Majimaji.
2.kagera
sugar 1-0 Stand United
Mfungaji ni Mbaraka Yusuph
3.Ndanda
0-2 Mtibwa Sugar
Wafungaji ni vicent barnabas na Haruna Chanongo
4.Mwadui
1-0 Mbao
Mfungaji Awadh Juma
5.
Mbeya city 0-0 Toto Africa
Msimamo wa Ligi Kuu Msimu Huu
Rn | Timu | P | W | D | L | F | A | Gd | Pts |
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
1 | SIMBA SC | 17 | 13 | 2 | 2 | 29 | 6 | 23 | 41 |
2 | YANGA | 17 | 11 | 4 | 2 | 35 | 9 | 26 | 37 |
3 | KAGERA SUGAR | 17 | 8 | 4 | 5 | 17 | 16 | 1 | 28 |
4 | Azam FC | 17 | 7 | 6 | 4 | 24 | 15 | 9 | 27 |
5 | MTIBWA SUGAR | 17 | 7 | 6 | 4 | 22 | 19 | 3 | 27 |
6 | STAND UNITED | 17 | 5 | 7 | 5 | 15 | 14 | 1 | 22 |
7 | T. PRISONS | 16 | 5 | 7 | 4 | 10 | 10 | 0 | 22 |
8 | MBEYA CITY | 17 | 5 | 6 | 6 | 13 | 15 | -2 | 21 |
9 | Ruvu Shooting | 16 | 4 | 8 | 4 | 15 | 17 | -2 | 20 |
10 | African Lyon | 17 | 4 | 7 | 6 | 11 | 16 | -5 | 19 |
11 | MWADUI FC | 17 | 5 | 4 | 8 | 14 | 21 | -7 | 19 |
12 | NDANDA FC | 17 | 5 | 4 | 8 | 13 | 20 | -7 | 19 |
13 | Mbao FC | 17 | 5 | 3 | 9 | 16 | 21 | -5 | 18 |
14 | MAJIMAJI FC | 17 | 5 | 2 | 10 | 13 | 25 | -12 | 17 |
15 | TOTO AFRICANS | 17 | 3 | 4 | 10 | 9 | 18 | -9 | 13 |
16 | JKT RUVU | 17 | 2 | 7 | 8 | 6 | 16 | -10 | 13 |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni