![]() |
Viongozi wa Simba SC wamepania kutengeneza kikosi kikali kuelekea msimu ujao |
UONGOZI wa klabu ya Simba imenasa vifaa kutoka Botswana na Senegal ambapo watawapima kusaka mchezaji mmoja atakayeziba nafasi moja ya mchezaji wa Kimataifa iliyobaki wazi.
Simba imebakisha nafasi moja kukamilisha usajili wa wachezaji wa Kimataifa ambapo hadi sasa imeishasajili wachezaji Amis Tambwe, Joseph Owino, Kwizera Pierre na Modo Kiongore.
Akizungumza
Dar es Salaam jana, Makamu wa Rais wa Simba Geofrey Nyange ‘Kaburu’
alisema wachezaji hao ni Jerom JJ anayetokea timu ya Taifa ya Botswana
na Osumani Mane ambaye anachezea Senegal akiwa ni raia wa Gambia ambapo
kocha mkuu wa Simba Zdravko Logarusic ataangalia viwango vyao na
kupendekeza mchezaji mmoja ambaye watamsajili.
“JJ atawasili leo (kesho) wakati Mane anatarajia kuwasili leo (jana) wote wakichezea nafasi ya Mshambuliaji na ndiyo nafasi tunayosaka mchezaji wa kuiziba hivyo kocha ataangalia uwezo wa kila mmoja na atakayeridhika naye tutamchukua na kuingia nae mkataba,” alisema.
Alisema, Loga atawapima wachezaji hao katika kambi watakayoweka Zanzibar siku ya Jumatatu ambayo itakuwa ya wiki tatu au nne ambapo pia itakuwa ni nafasi nzuri ya kocha kukisoma kikosi chake chote kabla ya kuingia katika ligi.
Alisema, kocha amependekeza atafutiwe mechi tatu za kirafiki za Kimataifa watakazojipima nazo zenye uwezo wa juu.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni