
Pep Guardiola amemuorodhesha kiungo wa Manchester United Ander Herrera
kwenye list ya wachezaji wapya ambao huenda akafanyanao kazi kwenye timu ya Manchester City ambayo anajiandaa kwenda kuchukua mikoba ya Manuele Pellegrin.
Baadhi ya Wachezaji wa Manchester United wanataka kocha wa Atletico Madrid Diego
Simeone akafundishe timu hiyo endapo kocha wao wa sasa Louis van Gaal akiondoka kwenye timu hiyo.
Jurgen Klopp amewashauri Liverpool wafanye kila wawezalo ili kumsajili kiungo wa Real Madrid Toni Kroos kwenye kipindi hiki cha usajili baada ya mchezaji huyo wa kimataifa kutoka Germany kushindwa kupata nafasi chini ya Rafa Benitez.
Juventus wapo tayari kuongeza dau la paundi milioni 30 kwa lengo la kumsajili kiungo wa Ilkay Gundogan wa Borussia Dortmund.
Kocha wa Manchester United Louis van Gaal yupo kwenye mpango wa kusitisha mkataba wa muda mfupi kwa Adnan
Januzaj aliyemtoa kwa mkopo kwenye timu ya Borussia Dortmund na kumrejesha Old Trafford ili kuongeza nguvu kikosini.




Hakuna maoni:
Chapisha Maoni