Cristiano Ronaldo na Gareth Bale wakishangilia baada ya Mreno huyo kufunga goli lake la pili
MWANASOKA bora wa dunia na Ulaya,
Cristiano Ronaldo amepiga 'hat-trick' na goli ya nyongeza (magoli 4)
Real Madrid ikiitandika Elche 5-1 katika mechi ya ligi kuu nchini
Hispania, La Liga.
Goli lingine lilifungwa na mchezaji ghali zaidi duniani Gareth Bale
Kikosi cha Carlo Ancelotti kimefunga mabao 18 katika mechi tatu.
Magoli ya jana yamemfanya Ronaldo
afikishe mabao 8 ndani ya wiki moja na baada ya mechi aliulizwa kama
bado ana furaha Real madrid.
Alisema: "Binafsi mambo yanakwenda vizuri, timu inafunga magoli, inashinda mechi na kucheza vizuri."
Aliulizwa kuhusu maneno ya hivi karibuni
aliyosema Jose Mourinho kwamba wawili hao hawana mahusiano mazuri,
alisema: "Sio wajibu wangu kuzungumza mambo kama hayo, mimi naangalia
zaidi ninachokifanya uwanjani."
Mshambuliaji wa Elche, Edu Albscar
(kulia) akifunga penalti matata iliyofungua mvua ya magoli, huku kipa
Keylor Navas akijaribu kuokoa bila mafanikio.
Bale akishangilia goli lake
Ronaldo akitia kambani goli katika mechi 13 mfululizo za nyumbani
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni