Fernando Torres akishangilia bao lake la kwanza akiwa AC Milan
FERNANDO Torres amefungua goli la kwanza
AC Milan ikitoka nyuma na kupata sare ya 2-2 dhidi ya timu iliyopanda
ligi kuu ya Italia, Seria A, Empoli.
Baada ya goli la mapema la Lorenzo Tonelli na Manuel Pucciarelli, Torres alifunga kwa kichwa katika dakika ya 43 na Mjapan Keisuke Honda alisawazisha bao lingine katika dakika ya 58.
Milan walikuwa na nafasi ya kushinda
baada yaTorres aliyejiunga kwa mkopo wa miaka miwili mwezi uliopita
kutoka Chelsea kumtengenezea nafasi Jeremy Menez katika dakika ya 62,
lakini shuti la Mfaransa huyo liligonga mwamba.
Mshambuliaji wa zamani wa Chelsea alipiga kichwa cha hatari na kutia kambani mpira.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni