Arsenal walifungwa 2-0 na Dortmund siku ya jumanne, lakini bado wana imani kubwa ya kufanya vizuri
BADO ni mapema mwa msimu, lakini tayari
kuna maswali ya kujiuliza kuhusu Arsenal. Swali kubwa ninalohisi ni hili
hapa: Kipi kinabadilika?
Kwa kuwatazama dhidi ya Borrussia Dortmund jumanne usiku, isingewezekana kuhitimisha kwamba, Arsenal hawajifunzi.
Kwa muongo mmoja sasa, Arsenal wamekuwa
wakishindwa kupambana na timu inayocheza mpira wa kasi na mpango wa
kutumia nguvu. Kila mtu anajua jinsi ya kucheza nao.
Danny Welbeck amesajiliwa kutoka Manchester United, lakini bado amekuwa na ugonjwa wa kukosa nafasi za magoli.
Dortmund wangeweza kufunga mabao
kirahisi kama walivyofanya Liverpool (5-1 mwezi februari) na Cheslea
(6-0 mwezi machi), lakini kitendo cha kutofungwa mechi 29 za ugenini
katika michuano ya UEFA, kiukweli ni rekodi nzuri mno kwa Arsenal.
Ninapoitazama Arsenal kwasasa,
ninachanganyikiwa. Wanacheza vilevile kila wanapokwenda- mabeki wao wa
pembeni wanapanda juu na kutanuka- na hufungwa kwa mashambulizi ya
kushitukiza.
Wao ni wageni! wangekuwa wanafanya hivyo wakiwa nyumbani. Kwanini hawajifunzi?
Nilipokuwa naichezea Liverpool, lengo la
kwanza siku zote lilikuwa kutofungwa: Tulijilinda sana na kama nafasi
inatokea basi tuliitumia haraka. Kama mashabiki wa nyumbani hawakupenda,
maana yake ilikuwa nini?
Bado Arsenal wanaamini wanaweza kuifunga
timu yoyote na popote pale wakicheza mpira wao. Ni vibaya sana. Timu
pekee iliyoweza kushinda ugenini kwa miaka ya karibuni kwa staili hii ni
Barcelona ya Pep Guardiola. Moja ya timu kubwa zaidi miaka ya karibuni,
lakini alionekana kuja na mbinu nyingine za kutafuta matokeo.
Angalia mabingwa wa mwaka jana wa UEFA,
Real Madrid, walifuzu fainali kwa kushambulia kwa kushitukiza dhidi ya
Bayern Munich-na hii ilikuwa katika mchezo wa kwanza Bernabeu. Ilikuwa
mbinu nzuri kwao.
Kufanya mambo tofauti ni jambo la msingi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni