MCHEZAJI wa soka nchini
Uganda Fahad Musana ameanguka na kufariki muda mchache baada ya Frank
Lampard kufunga bao kusawazisha katika mchezo wa Ligi Kuu nchini
Uingereza kati ya Manchester City na Chelsea. Kifo cha Musana mwenye
umri wa miaka 24 kimekuja kwa mshtuko hususani baada ya beki huyo
kucheza mechi yote katika ya klabu yake ya Simba iliyoshinda bao 1-0
dhidi ya Entebe FC katika mchezo wa Ligi Kuu nchini Uganda uliofanyika
katika Uwanja wa Nakivubo. Kwa mujibu wa kocha wa Simba Fred Kajoba,
Musana pia alifanya mazoezi na timu siku ya jana asubuhi katika viwanja
vya Bombo na hakuonyesha tatizo lolote. Shirikisho la Soka la
Uganda-FUFA lilituma taarifa za kifo hicho cha ghafla jana usiku ambapo
mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya Barracks iliyopo huko
Bombo kwa ajili taratibu za mazishi. Shuhuda aliyekuwepo eneo ambalo
Musana alikuwa akitazama mechi hiyo amesema mchezaji huyo alikuwa
akifurahia mchezo huo mpaka ilipofikia hatua ya Lampard aliposawazisha
ndipo alipoanguka ghafla ya kukimbizwa hospitali ya Jeshi ya
Bombo. Inaarifiwa kuwa mbali na kupenda kucheza kamari, Musana alikuwa
shabiki wa kutupwa wa Chelsea na alikuwa yuko tayari kufanya lolote kwa
ajili ya timu hiyo. Mashabiki wa soka la Uingereza nchini Uganda
wamekuwa wakipata matukio katika miaka ya karibuni ambapo mwaka jana
mshabiki wa klabu ya Arsenal aliripotiwa kupoteza nyumba baada ya kuweka
kamari kwamba timu hiyo ingeifunga Manchester United katika mchezo wa
Ligi Kuu lakini matokeo yake wakafungwa bao 1-0.
TANGAZA NASI: +255 655 442 255
CHANZI OPEN SCHOOL
Jumatatu, 22 Septemba 2014
Home
/
Unlabelled
/
MCHEZAJI WA LIGI KUU UGANDA AFARIKI GHAFLA KUFUATIA BAO LA KUSAWAZISHA LA LAMPARD JANA.
MCHEZAJI WA LIGI KUU UGANDA AFARIKI GHAFLA KUFUATIA BAO LA KUSAWAZISHA LA LAMPARD JANA.
About asantemuya
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA
Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni