STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumamosi, 20 Septemba 2014

SAMATTA NA ULIMWENGU KATIKA MECHI NZITO TP MAZEMBE UGENINI LEO

KLABU ya Entente Setif ya Algeria insignia kwenye mechi ya kiasi dhidi ya TP Mazembe katika Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika leo Uwanja wa Stade du 8 Mai 1945 usiku wa leo.
Huo utakuwa mchezo wa pili kuzikutanisha timu hizo mfululizo kwa michuano ya Afrika, baada ya awali kukutana mwaka jana katika hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho.
Mazembe haikufungwa na Setif katika Kundi B wakitoa safe ya 1-1 nchini Algeria kabla ya kuwafunga 4-2 mjini Lubumbashi. 
Mbwana Samatta anatarajiwa kuendelea kuibeba Mazembe leo
Setif ilishika mkia katika Kundi B wakati Mazembe ilikwenda Nusu Fainali ambako walitolewa na CS Sfaxien ya Tunisia kwenye fainali kwa kufungwa 1-0 matokeo ya jumla.
“Tutajaribu kulipa kisasi cha kufungwa 4-2 msimu uliopita, na pia tulikutana nap katika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa mwaka 2010,” alisema kocha wa Setif, Kheireddine Madoui.
Setif haijafungwa katika Ligi ya Mabingwa msimu huu chini ya kocha mwenye umri wa miaka 37 na ilitinga Nusu Fainali baada ya sare nne na kushinda mechi mbili kwenye kundi lake.
Wakati huo huo, Mazembe haina rekodi ya uhakika ya mechi za ugenini, imefungwa mara mbili na kutoa sare tatu katika mechi zake tano za ugenini mwaka huu.
Lakini kiungo Rainford Kalaba, anaamini wanaweza kushinda mechi yao ya kwanza ugenini leo tangu Machi, 2013 walipoichapa Centre Chiefs of Botswana 1-0.
"Moyoni mwangu, naweza kufikiria kitu hicho tu: Kwenda Setif kushinda. Mechi za Nusu Fainali zina uzito tofauti, kwa sababu  zinafungua milango ya fainali," amesema Kalaba.
Washambuliaji wawili Watanzania, Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu wanatarajiwa kuendelea kuibeba Mazembe leo. 
Nusu Fainali nyingine ni kati ya AS Vita ya DRC dhidi ya CX Sfaxien ya Tunisia mjini Kinshasa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox