WAKATI
Arsenal wakitinga hatua ya 16 Bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya
kupata ushindi nyumbani, Liverpool imejikuta ikibanwa ugenini kwa
kuambulia sare.
Arsenal
walipata ushindi muhimu nyumbani dhidi ya Borussia Dortmund kwa
kuwalaza mabao 2-0 wakati Liverpool ililazimishwa sare ya 2-2 na Ludogorets .
Mabao
ya Yaya Sanogo na jingine la Alexis Sanchez yalitosha kuivusha Arsenal
hatua hiyo katika mechi kali iliyochezwa uwanja wa Emirates.
Arsenal
imeungana na Wajerumani hao kutinga hatua ya 16 Bora kutoka kundi D
baada ya kufikisha pointi 10, tatu nyuma ya Dortmund inayoongoza
kileleni.
Nao Liverpool ililazimishwa sare ya 2-2 na Ludogoretsna kuzidi kujiweka pabaya katika azma yao ya kucheza hatua ya mtoano.
Ludogorets
waliwashtukiza wageni wao kwa kupata bao la mapema la dakika tatu
kupitia Dani Abalo kabla ya Liverpool kusawazisha dakika tano baadaye
kupitia Rickie Lambert na baadaye Jordan Henderson kuwapa uongozi wa 2-1
wageni.
Hata
hivyo Vijogoo vya England walishindwa kulinda bao lao baada ya kuruhusu
wenyeji kusawazisha dakika mbili kabla ya mchezo huo kumalizika baada
ya Georgi Teziev kuifuingia Lodogorets.
Sare
hiyo imeifanya Liverpool kufikisha pointi nne na kushika nafasi ya tatu
ikitanguliwa na Basel iliyolazwa bao 1-0 na Real Madrid iliyotangulia
16 Bora ikiongoza kundi B.
Bao la Real lilifungwa na Ronaldo na kumfanya Mreno huyo kumfikia Raul katika orodha ya waliofunga mabao mengi katika ligi hiyo wakishika nafasi ya pili nyuma ya Lionel Messi anayeongoza kwa mabao 74 dhidi ya 71 na wakali hao.
Bao la Real lilifungwa na Ronaldo na kumfanya Mreno huyo kumfikia Raul katika orodha ya waliofunga mabao mengi katika ligi hiyo wakishika nafasi ya pili nyuma ya Lionel Messi anayeongoza kwa mabao 74 dhidi ya 71 na wakali hao.
Katika
mechi nyingine Zenit iliitambia Benfica kwa kuilaza bao 1-0, huku
Atlético Madrid ikiendeleza rekodi yao ya kutofungwa uwanja wa nyumbani
kwa kuicharaza Olympiakos Pirates kwa mabao 4-0 na kufuzu 16 Bora.
Wakali
wa Italia, Juventus wakipata ushindi muhimu ugenini dhidi ya Malmo,
huku Monaco ikiwa ugenini ilipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Bayer
Leverkusen, huku Anderlecht ikiinyoa Galatasaray kwa mabao 2-0.
Mpaka
sasa wakati michuano hiyo ikisaliwa na raundi moja kabla ya kufikia
tamati hatua ya makundi timu nane ndizo zimejihakikisha hatua inayofuata
zitakazochezwa mwezi ujao.
Timu
hizo ni pamoja na Atletico Madrid, Real Madrid na Barcelona zote za
Hispania, Chelsea na Arsenal za England, Bayern Munich na Borussia
Dortmund za Ujerumani, PSG ya Ufaransa, POrto ya Ureno na Shakhtar
Donetsk ya Uturuki.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni