MENEJA wa zamani wa Tottenham Hotspurs, Harry Redknapp amedai kuwa Manchester United wameshakamilisha mazungumzo ambayo yatamfanya Jose Mourinho kuwa meneja mpya ajaye katika klabu hiyo.
Mourinho amekuwa akitajwa kama chaguo sahihi kwa United kutokana na meneja wa sasa Louis van Gaal kushindwa kupata matokeo mazuri.
Van Gaal mwenyewe amedai United hawawezi kufanya mzungumzo na Mourinho bila kufahamu lakini Redknapp amesema tayari dili la ujio wake limeshakamilika.
Akihojiwa Redknapp amsema Van Gaal hajapata mafanikio yeyote toka atue United hivyo itakua vigumu kwa viongozi wa klabu hiyo kumvumilia.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni