STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumatano, 17 Februari 2016

TIZAMA HAPA MAMBO MAKUBWA MANNE YALIOJITOKEZA KWENYE MCHEZO WA PSG NA CHELSEA.......

http://en.parisinfo.com/var/otcp/sites/images/media/1.-photos/01.-ambiance-630-x-405/parc-des-princes-facade-630x405-c-otcp-dr/163898-1-fre-FR/Parc-des-princes-facade-630x405-C-OTCP-DR.jpg
                                      STORI YA KWANZA
 Usiku wa February 16 ulikuwa ni wa Ulaya (UEFA Champions League) ambap[o ilipigwa michezo miwili ya hatua ya mtoano (16 bora). PSG ilikuwa kwenye uwanja wake wa nyumbani Parc des Princes kuikabili Chelsea huku Benfica nayo ikiwa kwenye dimba la Estádio da Luz kupambana na Zenit St Petersburg
 Ibrahimovic 3

Mchezo uliopewa uzito wa juu ni wa PSG vs Chelsea kutokana na uhasimu ambao umekuwepo kati ya timu hizo mbili ambazo jana zilikuwa zikikutana kwa mara ya 16 kwenye ligi ya mabingwa Ulaya.

Katika mchezo huo ambao ulimalizika kwa PSG kuichapa Chelsea kwa bao 2-1, mchezaji Zlatan Ibrahimovic alifunga bao la kwanza kwenye mchezo huo na kuandika rekodi mpya kwenye maisha yake ya soka.

 Zlatan Ibrahimovic swaps shirts with Pedro AND Willian after Paris Saint-Germain edge

Superstar huyo wa Sweeden aliipatia PSG bao la kuongoza dakika ya 39 dhidi ya Chelsea kwenye mchezo huo wa kwanza wa mtoano hatua ya 16 bora.

Ibra ilipacika mpira kwenye nyavu za Chelsea baada ya free-kick yake kumgonga John Obi Mikel na kutinga wavuni huku golikipa Thibaut Courtois akipotea vibaya na kushindwa kuuokoa.

Baada ya kupachika bao dhidi ya Chelsea, Ibrahimovic amefikisha mabao 46 kwenye michezo ya ligi ya mabingwa barani Ulaya.

Lakini kiamini usiamini, goli la usiku wa jana lilikuwa ni goli lake pekee kufunga kwa mpira wa adhabu ndogo (free-kick) kati ya magoli yote 46.
 


Goli la Ibra limemfanya aingie kwenye rekodi ya wafungani bora wa muda wote wa Champions League pamoja na European Cup akilingana magoli na wakali kama mkongwe wa Ureno Eusebio, Karim Benzema na Filippo Inzaghi lakini wote hao wanatofautishwa na mechi walizocheza huku Ibra akiwa ameheza mechi nyingi zaidi kuliko wengine (116) .

Lakini pia, Zlatan Ibrahimovic amefunga kwenye mechi tatu za mwisho mfululizo za Champions League wakati huohuo amehusika kwenye kupatikana kwa magoli tisa kwenye mechi 11 za mwisho ilizocheza PSG kwenye mashindano yote. (magoli 7, assists 2)
 
 
                          STORI YA PILI 
 
 
Eden Hazard alikaririwa akisema kwamba haitokuwa jambo jepesi kuikataa ofa ya Paris Saint Germain ikitokea klabu hiyo ikimtaka.

  Hakuna cha kushangaza ukizingatia klabu inayotajwa ni tajiri na tayari imeshajihakikishia ubingwa wa Ufaransa kaa misimu kadhaa ijayo.

  
Kujiunga na PSG ni passport ya kwenda kucheza Champions League kila mwaka, na vile yeye ni mbelgiji – basi maisha yake ndani ya Paris yatazidi kuwa mepesi. Wanaongea lugha moja.

Lakini wakati tulipoitazama PSG jana usiku wakicheza dhidi ya Chelsea pale Parc des Princes, unapata mawazo kwamba wakati Hazard ana matamanio ya kwenda PSg, je boss wa klabu hiyo Laurent Blanc anamhitaji Hazard kwenye kikosi chake.

Katika wiki za hivi karibuni mchezaji huyo wa zamani wa Lille amekuwa akirejea kutoka kwenye majeruhi ya hip, lakini kasi ya kurudisha kiwango chake imekuwa kama ya funza. Huku akiendelea kuvuta paundi laki mbili kila mwisho wa wiki.

Bado anavaa jezi yake nambari 10 ambayo amekuwa akiipenda kwa muda mrefu. Na kikubwa zaidi hivi sasa anacheza chini ya kocha ambaye hampi majukumu mazito katika kukaba kama ilivyokuwa kwa kocha aliyepit Jose Mourinho ambaye alifukuzaa miezi kadhaa iliyopita.

Huu ulipaswa kuwa muda sahihi kwa Hazard kurudi kwenye kiwango chake na kuibeba timu hake inayosuasua.

  

 Lakini imekuwa tofauti na ushahidi ni mechi ya jana, alikuwa ‘flop of the game’ – akifunikwa kwenye mchezo mkubwa – mahala ambapo anaamini ndipo anapostahili kuonyesha umwamba wake.

Kivuli cha Hazard wa zamani – alikuwa ni mchezaji aliyevaa jezi za blue wa PSG – mbrazil Lucas Moura.

Lucas na Hazard – wote wana sifa zinazofanana kimaumbo – 5ft 6in na 10st, lakini wakiwa wnacheza kwa majukumu tofauti, mbrazil huyo ndio aliyekuwa akiichachafya mno safu ya ulinzi ya Chelsea namna ambavyo Hazard alikuwa anazifanya safu za ulinzi za timu nyingine miezi kadhaa nyuma.

Usiku wa jana mwanasoka huyo bora wa Premier league msimu uliopita alipewa ukumbusho kwamba labda Mr Jose Mourinho alikuwa sahihi kusema wachezaji wa aina ya Hazard hawaruhusiwi kuwa na msimu m’baya.

Lucas Moura aliwapa shida mabeki wa Chelsea – katika dakika zote alizocheza alikuwa kila mahala.

  

 Dakika mbili tu baada ya mchezo kuanza, yeye na Zlatan walishirikiana vizuri na almanusra waipe timu yao uongozi wa mapema kwenye mchezo huo.

Dakika 4 baadae alileta balaa lingine kwenye safu ya ulinzi ya Chelsea akiwa yadi 25 kutoka kwenye goli, kasi yake na nguvu ilikuwa silaha kubwa kwa PSG jana.

Akihama kutoka kushoto kwenda kulia, akicheza nyuma ya mshambuliaji wa kati Ibrahimovic, alifanya kila
kitu katika kuidhuru Chelsea.


Alipewa majukumu mazito kwa hlande wake ila kwa watazamaji tulikuwa tunaenjoy – Hazard jaa upande wake alikuwa kama miguuni kafungwa vyuma.

Alipiga pasi kadhaa nzuri, na utundu kiasi lakini alikuwa na mchango mdogo sana katika kuihakikishia timu yake inatoka na matokeo chanya Paris.

Hukuhitaji kujua kuongea kiingereza, kifaransa au kiitaliano kusoma na kuelewa kitu gani kilikuwa kichwani mwake – lugha ya mwili wake ilitoa majibu yote.

Hali hii ilikuwa hivyo hivyo katika mchezo wa jumamosi pale Stamford Bridge wakati kila mchezaji alijisaidia kupata sifa katika mechi dhidi ya vibonde Newcastle na matokeo wakapata ushindi wa 5-1, lakini Hazard akaonyezha kiwango cha chini.

Mbelgiji huyu ameifungia Chelsea goli moja tu msimu huu tena dhidi ya klabu ya MK Dons katika kombe la FA Cup.

Lucas Moura amefunga magoli 8. Sawa, inawezekana kwenye ligi nyepesi tofauti na EPL lakini ameendelea kuonyesha anaweza kufanya vizuri kwenye mechi kubwa pia kama jana usiku.

Moura alisababisha faulo ambayo ilipelekea goli la kwanza la PSG lilofungwa na Zlatan Ibrahimovic.

Kasi yake ya hatari ilimzidi ujanja Mikel Obi ambaye hakuwa na namna zaidi ya kumfanyia madhambi nje ya eneo la hatari.

Moura aliendelea kuikimbiza safu ya ulinzi ya Chelsea, Hazard akatolewa dakika ya 71 akijua kabisa amefunikwa kwenye mchezo ambao ungewashawishi PSG kutuma ofa ambayo yeye asingeweza kuikataa.

Kwa Hazard huyu wa sasa – sioni namna gani PSG watatuma ofa ambayo hatoweza kuikataa.

                          STORI YA TATU 


chels
Inasemekana kwamba Chelsea hawajapata kipigia cha magoli 2-1 peke yake bali walikutana na gesi ya kutoa machozi pale pale ndani ya uwanja. 

 Kwenye mechi ambayo imechezwa kwenye uwanja wa Parc Des Princes kati ya PSG Vs Chelsea askari wa France walitumia mabomu ya machozi kwa mwaka wa pili mfululizo Chelsea wanavyocheza uwanjani hapo.

Kuna mashabiki ilibidi waondoke kipindi cha kwanza hata kabla Mikel Obi hajafunga goli la kusawazisha kutokana na moshi uliotokana na kupulizwa kwa gesi hiyo hapo uwanjani.

Sababu kubwa ya kupulizwa hiyo gesi ni kwa ajili ya kutuliza fujo lakini askari mmoja alisema imepulizwa kwa bahati mbaya kwasababu hakukua na fujo yoyote iliyohitaji kupulizwa hiyo gesi hapo uwanjani.

Lakini baada ya Mikel Obi kufunga goli la kusawazisha na ushangiliji kuendelea kwa kasi muda wa mapumziko, kukatoea tishio la kupulizwa tena gesi hiyo kutoka kwa askari waliokuwepo hapo uwanjani.

Pia kulikua na fujo nyingi nje ya uwanja ambazo zilisababishwa na mashabiki wa Chelsea. Mfano kuna video imerekodiwa ikiwaonyesha mashabiki wa Chelsea wakimzuia mtu mmoja kuingia kwenye treni. Hapo walikua na hasira zao baada ya mechi ya kuisha kwa 2-1.
 
                                                        VIKOSI;
 
PSG (4-3-2-1): Trapp 7.5; Marquinhos 7, Thiago Silva 7, Luiz 6.5, Maxwell 7; Verratti 8 (Rabiot 81, 6), Thiago Motta 8, Matuidi 8.5 (Pastore 81, 6); Di Maria 7, Lucas Moura 7 (Cavani 74, 7); Ibrahimovic 7.
 
 
 
Subs not used: Sirigu, Stambouli, Kurzawa, Van der Wiel.
Booked: Ibrahimovic, Luiz, Lucas.
Goals: Ibrahimovic 39, Cavani 78. 
Manager: Laurent Blanc 7.5. 
 
 
 
Chelsea (4-1-4-1): Courtois 7.5; Azpilicueta 6.5, Ivanovic 8, Cahill 8, Baba 7; Mikel 7; Pedro 6.5, Willian 7.5, Fabregas 7, Hazard 6.5 (Oscar 71, 6); Costa 7.
 
Subs not used: Begovic, Traore, Kenedy, Remy, Miazga, Loftus-Cheek.
Booked: Mikel, Pedro. 
Goal: Mikel 45+1. 
 
Manager: Guus Hiddink 7. 
Referee: Carlos Velasco Carballo 6.5.
Man of the Match: Blaise Matuidi. 
 
                 WAGENI MASHUHURI 
 
Ronaldo was one of many famous faces in the French capital to watch Paris Saint-Germain take on Chelsea
Ronaldo de Lima ni miongoni mwa watu walioshuhudia mchezo wa Psg na Chelsea
Ronaldo waves to supporters who haven't forgotten the former striker's past goal scoring exploits

Former PSG boss Carlo Ancelotti was also in attendance with his wife Mariann Barrena McClay
 Carlo Ancelotti akiwa na mke wake  Mariann Barrena McClay
Ancelotti also found time to catch up with France manager Didier Deschamps who watched the game close by
Ancelotti akiteta na kocha wa timu ya taifa ya Ufaransa  Didier Deschamps
Deschamps aims to lead France to home glory at Euro 2016 this summer but only one French player started for Paris Saint-Germain in their 2-1 last 16 victory over Chelsea

Former Manchester United manager David Moyes also bagged a ticket for the return of the Champions League
 David Moyes akitizama mchezo wa Psg na Chelsea
Moyes has been out of a managerial job since being sacked by Real Sociedad in November

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox