STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Alhamisi, 13 Novemba 2014

MESSI AFUNGA BAO LA USHINDI ARGENTINA IKIICHAPA 2-1 CROATIA KWA MBINDE ENGLAND

ARGENTINA imeshinda 2-1 kwa mbinde dhidi ya Croatia katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa usiku wa kuamkia leo Uwanja wa Upton Park, England.   
Washindi hao wa pili wa Kombe la Dunia Julai mwaka huu, walilazimika kutoka nyuma ili kupata ushindi huo, baada ya Anas Sharbini kuifungia Croatia bao la kuongoza dakika ya 11.
Argentina ilipata bao la kusawazisha kupitia kwa Cristian Ansaldi dakika ya 48, kabla ya Lionel Messi kufunga la ushindi kwa penalti dakika ya 57 kufuatia Sergio Aguero kuangushwa kwenye eneo la hatari.
Mshambuliaji Carlos Tevez alipata mapokezi mazuri aliporejea Upton Park  baada ya kuingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Aguero. 
Kikosi cha Argentina kilikuwa: Romero, Zabaleta, Vergini, Fazio, Ansaldi/Silva dk76,
Perez
, Mascherano, Banega/Pereyra dk70, Di Maria/Lamela dk76, Messi na Aguero/Tevez dk61.
Croatia: Lovre Kalinic/Vargic dk88, Vrsaljko, Leskovic/Mitrovic dk83, Jedvaj, Badelj, Leovac, Milic/Tomecak dk70, Kovacic/Halilovic dk46, Antolic, Sharbini/Jajalo dk64 na Cop/Rog dk83.
Messi shows off his skills as he takes on the Argentina defence 
Messi akiwatoka wachezaji wa Croatia katika mchezo huo 
Tevez waves to the Upton Park crowd from the bench after having spent a year at West Ham
Tevez akiwapungia mkono mashabiki Uwanja wa Upton Park, ambao wanamfahamu kwa sababu aliwahi kuchezea West Ham

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox