Uongozi
wa timu ya Young Africans umetoa mapumziko ya wiki mbili kwa wachezaji
wake na benchi la Ufundi kabla ya kurejea tena kuanza mazoezi jumatatu
ya Novemba 24 mwaka huu, kujiandaa na mzunguko wa nane wa Ligi Kuu ya
Vodacom Tanzania bara na mechi ya Nani Mtani Jembe dhidi ya Simba SC
katikati ya mwezi Disemba mwaka huu.
Kocha
mkuu wa Young Africans mbrazil Marcio Maximo alitoa mapumziko hayo kwa
wachezaji wake, kufuatia baadhi ya wachezaji kuitwa na timu zao za Taifa
kwa ajili ya mechi za kalenda ya FIFA na wengine kujiandaa na michuano
ya Challenge Afrika Mashariki na Kati.
Wachezaji
wa Young Africans walioitwa timu za Taifa ni (Tanzania), Deo Munish
"Dida", Oscar Joshua, Kelvin Yondani, Nadir Haroub "Cannavaro", Saimon
Msuva na Mrisho Ngasa (Rwanda) Haruna Niyonzima, (Uganda) Hamis Kizza.
Aidha
kocha Maximo pamoja na wachezaji kutoka nchini Brazil kiungo Andrey
Coutinho na mshambuliaji Geilson Santos "Jaja" wako nchini Brazil kwa
ajili ya mapumziko mafupi kabla ya kurejea kuendelea na maandalizi ya
mechi za mzunguko wa nane.
Kocha
msaidizi Leonardo Neiva amebakia nchini Tanzania, ambapo kwa sasa
anaandaa programu ambayo itatumika kuanzia Novemba 24, 2014 pindi kikosi
kitakapoanza tena maandalizi ya kujiandaa na michezo itakayofuata.
Wachezaj
wote wanatarjiwa kuripoti Novemba 24, mwaka huu kwa ajili ya mazoezi ya
kujiandaa kumalizia mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom pamoja na
mechi ya Nani Mtani Jembe dhidi ya Simba SC.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni