Serikali ya Iraq inasema kuwa
vikosi vyake vimeuteka mji wa kazkazini wa Tikrit kutoka kwa wapiganaji
wa ki-sunni ambao walikuwa wameteka mji huo wiki mbili zilizopita
.Vyombo vya habari vya kitaifa vimesema kuwa wanajeshi wakisaidiwa na mizinga pamoja na ndege za
Waasi hao wamesema kuwa kulikuwa na mapigano makali katika mji huo na kwamba mashambulizi hayo hayakufua dafu.
Iwapo itathibitishwa ,utekaji wa mji wa Tikrit utakuwa hatua kubwa ya jeshi la Iraq tangu ISIS kuyateka maeneo mengi ya Iraq kazkazini mapema mwezi huu.
Serikali sasa inasema kuwa inajiandaa kuelekea mjini Mosul ambao ni mji wa pili kwa ukubwa nchini humo.
Wizara ya Ulinzi inasema kuwa ndege hizo 5 zenye uwezo wa kushambulia maeneo ya ardhini zitaaanza kuhudumu katika kipindi cha siku chache zijazo,huku nyingine zikitarajiwa kuwasili.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni