STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Alhamisi, 10 Julai 2014

MKALI WA KOMBE LA DUNIA ASAINI MIAKA MIWILI AZAM FC NA KUSEMA...


Hapa anacheza Kombe la Mabara dhidi ya Hispania
Nyota wa Haiti Leonel Saint-Preux akisaini Mkataba wa miaka miwili na Azam FC leo Dar es Salaam
Hapa anakabidhiwa jezi na Meneja wa Azam FC, Jemadari Said
Wakala wake, Gibby Kalule kushoto akimsaidia kuvaa jezi

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Haiti, Leonel Saint-Preux leo amesaini Mkataba wa miaka miwili kuichezea Azam FC kuanzia msimu ujao.
Nyota huyo aliyeicheza Haiti katika Kombe la Mabara ya Dunia la FIFA mwaka jana nchini Brazil, amesaini mchana huu baada ya kufanya vizuri katika majaribio ya wiki moja Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
“Nimefurahi kukamilisha usajili wangu, ni changamoto nyingine nzuri kwangu, natakiwa sasa kuthibitisha uwezo wangu uwanjani na kutumia uzoefu wangu wa kucheza mashindano makubwa duniani kuisaidia timu,”amesema.
Nyota huyo aliyewahi kuchezea APR ya Rwanda kwa miezi saba mwaka 2011, amesema kwamba anaweza kucheza katika mazingira yoyote na hana wasiwasi. Wakala wake, 
Gibby Kalule wa Uganda, amesema ana matumaini mchezaji wake atafanya vizuri Tanzania.
“Nina wachezaji wengi wazuri ambao watabadili soka ya Tanzania na kuleta msisimko zaidi, naanza na huyu, atakuwa balozi wangu mzuri hapa,”amesema.
Meneja wa Azam FC, Jemadari Said Kazumari amesema kwamba mchezaji huyo amemvutia kila mmoja kwa kipindi cha wiki moja alichokuwa na timu, hivyo wanasubiri kumuona msimu wa mashindano utakapoanza.  
Mshambuliaji huyo aliyezaliwa Machi 12, mwaka 1985 in Cap-Haitien mara ya mwisho alichezea klabu ya FELDA United F.C. ya Ligi Kuu ya Malaysia.
Kisoka, Saint-Preux alianzia Zenith ya kwao, ambako alikuwa mkali wa mabao katika Ligia ya nchini humo.
Saint-Preux alisaini Minnesota Thunder ya Daraja la Kwanza Marekani Aprili 15, mwaka 2009, kabla ya kuhamia Hanoi ya Vietnam.
Machi 2010 alisiani mkataba wa awali na Aztex, lakini akatemwa baada ya kueli vipimo vya afya.
Kimataifa Saint-Preux, alianzia kuchezea timu za vijana za Haiti wa umri tofauti. Alikuwemo kwenye kikosi cha Haiti kilichofuzu michezo ya Olimpiki mwaka 2008 mjini Beijing, akifunga bao la kukumbukwa kutoka umbali wa mita 40 timu yake ikishinda 2-1 dhidi ya Canada. 
Alianza kuchezea timu ya wakubwa ya Hati mwaka 2007. Alifunga bao lake la kwanza timu ya taifa ya Haiti Novemba 19, mwaka 2008 katika sare ya 1-1 Surinam. Haiti ilifungwa 10-0 na Hispania kwenye michuano hiyo. 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox