STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Alhamisi, 10 Julai 2014

SIMBA SC YAFANYA KUFURU, YASAINI WATATU KWA MPIGO LEO AKIWEMO MANYIKA JR. NA BEKI LA MWADUI

Said Tuliy kulia, Kaburu kushoto na Manyika Jr. katikati akisaini Simba SC

SIMBA SC imesajili wachezaji wawili chupukizi kwa ajili ya timu yake ya vijana chini ya umri wa miaka 20, maarufu kama Simba B, akiwemo Peter Manyika, mtoto wa kipa wa zamani wa Yanga SC, Manyika Opeter
Makamu Rais wa Simba SC, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ amesimamia zoezi hilo lililokamilika vyema akishirikiana na Mjumbe wa Kamati ya Usajili, Said Tuliy leo mjini Dar es Salaam.
Pamoja na kipa huyo wa timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20, Simba SC pia imemsajili kinda mwingine kutoka Mwadui ya Shinyanga, Ibrahim Hajibu Migomba.
Kaburu maarufu kama Perez, amesema mtoto wa Manyika amesaini miaka mitatu sawa na Hajibu ambao wote pamoja na kusajiliwa kama wachezaji wa Simba B, watakuwa wanakomazwa kikosi cha kwanza.
Awali ya hapo, leo Simba SC ilimsajili kipa wa Mtibwa Sugar ya Morogoro, Hussein Sharrif ‘Cassilas’ aliyesaini Mkataba wa miaka miwili.
Kaburu kushoto akiwa na Hajibu baada ya kusaini

Kipa huyo bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara amekuwa akiibeba Mtibwa Sugar kwa misimu mitatu iliyopita, tangu kuondoka kwa Shaaban Hassan Kado.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox