Msamaha: Hatimaye Luis Suarez amoeba radihi kwa kumng'ata beki wa Italian wiki iliyopita
MSHAMBULIAJI
Luis Suarez amepoza shutuma dhidi yake baada ya Jumatatu usiku
kuomba radihi kwa kumng'ata Giorgio Chiellini na ameahidi kutorudia
kufanya kosa kama hilo - huku Barcelona ikipiga hatua zaidi katika
kuwania saini yake.
Siku
nne baadea ya kufungiwa miezi minne na ameambia FIFA kwamba tukio hilo
lilitokea katika mechi ya Kombe la Dunia kati ya Uruguay na Italua mjini
Natal lilitokana na kushindwa kujizuia.
Mshambuliaji huyo wa Liverpool ameibuka kikamilifu na kujutia kosa lake. Lakini kuomba kwake radihi kunakuja katika wiki ambayo habari zimevuma mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 anatakiwa kwa dau la Pauni Milioni 80 Nou Camp.
Mshambuliaji huyo wa Liverpool ameibuka kikamilifu na kujutia kosa lake. Lakini kuomba kwake radihi kunakuja katika wiki ambayo habari zimevuma mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 anatakiwa kwa dau la Pauni Milioni 80 Nou Camp.
Gary
Lineker, mshambuliaji wa zamani wa Barcelona, amesema klabu hiyo ya
Katalunya imemuambia Suarez bombe msamaha kama wanataka waendelee na
jitihada za kumnunua.
Katika
taarifa yake aliyoitoa kwenye ukurasa wake wa Twitter, Suarez amesema:
"Baada ya siku kadhaa za kuwa nyumbani na familia yangu, nimepata fursa
ya kutuliza jazba na kufikiria haswa kilichotokea katika mechi ya Italia
na Uruguay Juni 24, 2014.
"Kutokana
na kilichotokea na yote yaliyofuatia baadaye, kiasi cha kuathiri hata
kiwango cha timu yangu ya taifa, ukweli ni kwamba mchezaji mwenzangu
Giorgio Chiellini ameumizwa na kilichotokea kwa kumng'ata,".
"Kwa
hili: Najuta kwa kiasi kikubwa kufanya hivyo. Naomba radhi kwa Giorgio
Chiellini na familia ya soka kwa ujumla. nauambia umma kwamba
halitatokea tukio kama hili tena,".
Beki
wa Juventus, Chiellini ameretweet msamaha wa Suarez katika mtandao
wake, baada ya awali kusema adhabu ya kumfungia miezi minne Suarez ni
kubwa.
Chiellini
amejibu kwenye akaunti yake ya Tweeter moja kwa moja akisema: "Yote
yamesahaulika. Natumai FIFA itakupunguzia adhabu,".
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni