Vijana
wawili wameuawa kwa kushambuliwa na wananchi wenye hasira mkoani Geita
kwa kile kilichotajwa kuwa vijana hao walimuua mama yao wa kambo kwa
kumcharanga mapanga sehemu mbalimbali za mwili wake.
Akizungumzia
tukio hilo kaimu Afisa mtendaji wa kata ya Busanda alisema tukio hilo
lilitokea jana katika kijiji cha Nyamtundu majira ya saa tatu usiku
ambapo Mama moja aliyejulikana kwa jina la Mwanamaila Mwanatenga (50)
aliuawa kwa kukatwa katwa mapanga na watu wasiojulikana wakati akitoka
chooni kujisaidia mara baada ya kumaliza kula.
Alisema
mara baada ya kufanya mauaji hayo walitokomea kusikojulikana na
wananchi kwa kushirikiana na jeshi la Sungusungu walianza msako wa
kuwatafuta na hatimaye waliwakamata wakijaribu kutoroka.
Watuhumiwa
hao walikamatwa katika kijiji jirani cha Msasa wakiwa na damu kwenye
makoti waliyokuwa wamevaa ndipo wananchi hao wakiwa na jeshi la
sungusungu waliwauliza kuwa wanatoka wapi.
Watuhumiwa
hao walijibu kuwa wanatoka kwenye sherehe ya harusi kwao na baada ya
wanafamilia kubaini kuwa mama yao wa kambo ameuawa walianza kuwapiga
hadi kuwaua na kisha wakawababua kwa moto.
Afisa huyo aliwataja waliokufa kuwa ni Makoye Nzari(25) na Masumbuko Nzari(36) wote wakiwa ni watoto wa kambo wa mama huyo.
Diwani wa kata hiyo Aliphonce Matonange amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.
Kamanda wa jeshi la polis mkoani Geita Joseph Konyo alisema hakuna aliyekamatwa juu ya tukio hilo na kwamba uchunguzi unaendelea wa kuwabaini waliofanya tukio hilo na huku akiwataka wananchi kuacha kujichukulia sheria mkononi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni