Mikel Arteta amateueliwa kuwa Nahodha mpya wa Arsenal
KOCHA Arsene Wenger amemthibitisha Mikel Arteta kuwa Nahodha mpya wa Arsenal kufuatia kumuuza Thomas Vermaelen kwa Barcelona FC.
Kocha
huyo wa The Gunners, ambaye aliishuhiudia timu yake ikiwafumua mabao
3-0 mabingwa wa England, Manchester City katika mchezo wa Ngao ya Jamii
jana, alilazimika kuwa na Nahodha mpya baada ya aliyekuwa Nahodha wake,
Vermaelen kutimkia Barcelona.
Mustakabli
wa Arteta katika klabu bado hauko wazi sana, lakini inaonekana kwa
kukabidhiwa uongozi wa wachezaji wenzake, mchezaji huyo mwenye umri wa
miaka 32 atabaki Arsenal msimu huu. Per Mertesacker ameteuliwa kuwa
Nahodha Msaidizi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni