STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumamosi, 16 Agosti 2014

HERRERA: MANCHESTER UNITED INASTAHILI KUWEPO LIGI YA MABINGWA


KIUNGO wa Manchester United, Ander Herrera amesema yeye na wachezaji wenzake wana malengo ya kuirudisha klabu hiyo nafasi ya juu katika soka la Ulaya.
Baada ya kumaliza katika nafasi ya saba msimu uliopita, United wanaanza kampeni za kusaka ubingwa wa England bila kushiriki michuano ya Ulaya kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1989-90.
Herrera ambaye alijiunga na United baada ya kuanguka mwaka 2013, anasisitiza kuwa kikosi cha Louis Van Gaal kinajipanga kufuta machungu ya msimu uliopita.
“Nisingeweza kuondoka Athletico kama nisingejiunga na klabu kama United,” Herrera aliwaambia The Guardian. “United ni fursa nzuri ambayo huwezi kukataa”.
“Niliiacha klabu ya kipekee, yenye falsafa maalumu na watu maalumu”
“Ni klabu ambayo wachache tunajivunia kuichezea, lakini kwa United naweza kukaa kwa miaka 10”.
“Hii ni klabu kubwa England, mpango mpya, wachezaji wapya na kocha mpya”

Herrera anatazamiwa kuanza mechi yake ya kwanza ya ligi kuu dhidi ya Swansea City leo jumamosi katika dimba la Old Trafford.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox