MENEJA wa klabu ya
Manchester United, Louis van Gaal amekiri baada ya kutoa sare ya bao 1-1
dhidi ya Sunderland kuwa alama moja katika mechi mbili za Ligi Kuu
walizocheza hazitoshi.
Akihojiwa kocha huyo raia wa Uholanzi amesema
wamepata alama moja na jambo hilo sio zuri kwa klabu kama hiyo.
Van Gaal
amesema wanatakiwa kufanya kazi kwa bidii zaidi kwani wacchezaji
wamesikitishwa na sare hiyo baada ya mchezo kwasababu walikuwa na
uhakika wa kushinda. Kocha huyo aliendelea kudai kuwa kwasasa wanahitaji
walau kushinda mechi moja ili kurejesha hali ya kujiamini halafu
wataona huko mbele watakavyokwenda.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni