Nyota wa Brazil , Neymar na Robinho wakionesha ufundi wao katika mazoezi mjini Miami.
BRAZIL wamerudi mazoezini kujiandaa na
mechi ya kesho ya kirafiki dhidi ya Colombia baada ya kuondolewa kwa
aibu katika fainali za kombe la dunia zilizofanyika majira ya kiangazi
mwaka huu katika ardhi yake.
Dunga, ambaye amerejea kwa mara ya pili
kuifundisha Brazil atawaongoza Selecao katika mchezo wa kwanza tangu
walipofungwa magoli 7-1 na Ujerumani katika mechi ya nusu fainali ya
kombe la dunia na mabao 3-0 dhidi ya Uholanzi katika mchezo wa mshindi
wa tatu mwezi julai mwaka huu.
Mabingwa hao mara tano wa dunia
wanafanya mazoezi mjini Miami wakiwa na nyota wao Neymar ambaye alipata
majeruhi makubwa katika mchezo wa robo fainali wa kombe la dunia dhidi
ya Colombia.
Amepona: Neymar alipata majeruhi katika mechi dhidi ya Colombia lakini amerudi uwanjani.
Bluu: Kiungo wa Chelsea, Willian, akitafuta kasi katika mazoezi ya Brazil
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni