STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumatatu, 8 Septemba 2014

CESC FABREGAS NA ARSENAL 'MAHABA NIUE', AFUNGUKA YA MOYONI KAMA CRISTIANO RONALDO KWA MAN UNITED!

  Kiungo Cesc Fabregas alijiunga na Chelsea akitokea Barcelona 

CESC Fabregas amekiri kuwa bado anajihisi kama mchezaji wa Arsenal-licha ya kujiunga na wapinzani wao wa London, klabu ya Chelsea kwa paundi milioni 30 majira ya kiangazi mwaka huu.
Kiungo huyo mshambuliaji wa Hispania tayari ameshaonesha makeke Stamford Bridge kwa kutoa pasi za mwisho nne kwa wachezaji wenzake msimu huu.
Baada ya kuondoka katika klabu yake aliyokulia ya Barcelona-Fabregas anatarajia kurudi katika klabu yake ya zamani ya London Kaskazini akiwa na uzi mpya wa Chelsea.
Enzi zake: Fabregas, ambaye aliichezea Arsenal kwa miaka 8, amesema siku zote anajihisi kama mchezaji wa Gunners
Furaha: Kiungo wa Hispania,  Fabregas (kushoto)  akishangilia bao la Chelsea dhidi ya Everton mapema msimu huu.
"Kwa wakati wote nitajihisi kama mtu wa Gunners na najua narudi pale (uwanja wa Emirates) na nahisi utakuwa wakati maalumu, lakini nimejifunga na Chelsea," Fabregas aliwaambia El Pais.
"Kumbuka nilicheza fainali ya ligi ya mabingwa dhidi ya Barcelona! naapa kwamba nilifanya kila kitu kuhakikisha tunashinda mechi ile hata kama nilikuwa Barcelona tangu utotoni"

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox