STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Alhamisi, 16 Oktoba 2014

WENGER ATOBOA SIRI YA MAJERUHI YA OZIL.

MENEJA wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger amebainisha kuwa Mesut Ozil alihisi tatizo katika goti lake katika mchezo dhidi ya Chelsea lakini aliendelea kucheza hivyo hivyo. Kiungo huyo alicheza dakika zote tisini katika mchezo huo waliofungwa mabao 2-0 lakini daktari wa Ujerumani alimuondoa katika kikosi cha timu ya taifa ya nchi hiyo baada ya kugundua kuwa kiungo huyo amechanika msuli wa ndani la goti lake ambao unaweza kumuweka nje kwa kipindi cha miezi mitatu. Wenger amesema anashangazwa na majeruhi ya wachezaji wake na kukiri kuwa anapata wakati mgumu kwani inaoenekana wachezaji wengi wenye majeruhi ya muda mrefu wameyapata bila hata kuguswa na mchezaji mwingine. Kocha huyo aliendelea kudai kuwa Ozil alilalamika kusikia maumivu kidogo wakati wa mapumziko na alimuambia daktari wao amuangalie na kama kutakuwa na tatizo lolote amuambie kwasababu tayari walikuwa nyuma kwa bao moja hivyo alihitaji wachezaji wote wa safu ya ushambuliaji. Wenger amesema kinachomshangaza ni kuwa Ozil hakugongana na mchezaji yeyote uwanjani, alikuwa akijaribu kutoa mpira kwa mwenzake ndipo alipoumia. Kutokana na majeruhi ya mara kwa mara yanayoiandama klabu hiyo baadhi ya wadau wamekuwa wakihoji mazoezi wanayopewa wachezaji hao lakini Wenger mwenyewe ametetea na kudai kuwa ni suala la bahati mbaya kwani wachezaji wake wengi waliopata majeruhi hivi karibuni yalitokana na wao wenyewe bila kuguswa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox