STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Ijumaa, 5 Desemba 2014

WALCOTT BADO MAJERUHI.

KLABU ya Arsenal itajitupa tena uwanjani kesho kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Stoke City bila ya winga wake Theo Walcott ambaye bado anauguza majeraha ya msuli. Walcott ambaye alirejea tena uwanjani na kucheza mechi mbili akitokea benchi Novemba mwaka huu naada ya kujiuguza kwa karibu mwaka mzima majeraha ya goti, aliumia msuli wakati akiwa katika majukumu ya kimataifa. Akizungumza na wana habari Wenger amesema Walcott alichomwa sindano leo hivyo hatakuwepo katika mchezo kesho na kuendelea kudai kuwa mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Galatasaray nao unaweza kuwa mapema sana kwake. Beki wa kushoto Nacho Monreal
pia
atakosa mchezo huo baada ya kuumia katika mchezo dhidi ya Southampton katikati ya wiki lakini golikipa Wojciech Szczesny yeye atakuwepo baada ya kuanza mazoezi. Mchezo huo unatarajiwa kuwa mgumu kwa Arsenal kwani toka Stoke wamepanda daraja mwaka 2008, washika bunduki hao wamefanikiwa kuwafunga mara moja pekee nyumbani kwao.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox