LISTI YA SIMBA VS MGAMBO... |
Watu
wengi hawapendi kukosolewa lakini wanaweza kuwa wavivu wa utekelezaji.
Kuna
mambo mengi yanahitajika kubadilishwa katika soka la Tanzania. Huenda mengine
yanaweza kuwa ya kipuuzi kabisa na hautegemei kuona yanaendelea lakini hakuna
anayeyafanyia kazi.
LISTI YA BARCELONA VS MAN CITY.... |
Kwanini
hawajayafanyii kazi? Jibu hawajali, hawaupendi mpira na wanachoangalia wao ni
kuingiza fedha kutoka katika mpira. Huu ni upuuzi.
Unapokuwa
jijini Dar es Salaam, mechi za Ligi Kuu Bara zimekuwa zikiandaliwa kwa
mpangilio mzuri sana.
Kitu
kidogo nitakupa mfano, karatasi ya listi ya wachezaji. Utaona imepangiliwa
vizuri kabisa tena kwa kuchapishwa.
Lakini
mechi nyingi za mkoani, karatasi zinachukuliwa zile za daftari au listi
inaandikwa hovyohovyo tu. Hauwezi ukasema hii ni hadhi ya Ligi Kuu Bara.
Karatasi
ya listi za wachezaji ya Ligi Kuu Bara, mechi kati ya Simba dhidi ya Mgambo
haina tofauti na mechi ya mchangani. Upuuzi.
Chama
cha Soka Tanzania, kinapata mgawo katika mapato ya mechi hiyo. Kununua karatasi
na kufanya mambo kwa mpangilio haiwezekani?
Hakuna
kiongozi anayeona hilo si sahihi, hawana aibu na wanakubali vipi ifanyike?
Kama
hao wanakubali, vipi uongozi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) nao unakubali
hali hiyo? Unaona sawa kwa kuwa mambo yanakwenda?
TFF inapaswa kuwa kiongozi anayeangalia uhakika na hadhi ya inachokiongoza. Mabadiliko yafanyike. Ala!
Source... saleh jembe
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni