STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumatano, 18 Machi 2015

SIMBA YACHEZEA VIRUNGU VYA MGAMBO

Mabingwa wa kombe la Mapinduzi Simba SC leo wameambulia kichapo toka kwa Mgambo shooting baada ya kupata ushindi mitatu mfululizo.

Simba SC leo walikuwa wageni wa Mgambo Shooting katika mchezo uliochezwa katika uwanja wa CCM Mkwakwani na kushuhudia Mgambo wakiibuka na ushindi wa goli 2-0.

Katika mchezo huo uliotawaliwa na mipira mirefu, Mgambo Shooting walikuwa wa mwanzo kuandika goli katika dakika ya 45 kufuatia shuti la mbali la Ally Nasorro na kuipeleka Mgambo mapumziko wakiwa mbele kwa goli 1-0.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku Simba SC wakitafuta goli la kufutia machozi, ambapo katika dakika ya 64 kipa wa Simba Ivo Mapunda alizawadiwa kadi nyekundu na kupelekea kutolewa kwa Said Ndemla na kuingia Manyika Peter.

Mapunda alipewa kadi nyekundu ya moja kwa moja baada ya kufanya madhambi katika eneo la hatari na kuzaa penati iliyo tiwa kimiani na Fullzulu Maganga na kuipa goli la pili Mgambo shooting na kupelekea mchezo kumalizika kwa Mgambo shooting kupata ushindi wa goli 2-0.

Ushindi huo umewafanya Mgambo shooting kufikisha pointi 24 na kupanda hadi nafasi ya 7 katika msimamo wa ligi kuu ya vodacom.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox