STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumatano, 18 Machi 2015

YANGA KILELENI KWENYE MSIMAMO WA LIGI KUU TENA



Wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya kimataifa Yanga leo wamefanikiwa kurejea kileleni mwa ligi kuu ya vodacom baada ya kuibuka na ushindi wa goli 2-1 dhidi ya Kagera Sugar katika mchezo uliochezwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Yanga walianza mchezo taratibu na Kagera sugar wakitawala mchezo huku yanga wakitumia zaidi mashambuliz ya kushtukiza ambapo katika dakika ya 7 walipata penati baada ya Amisi Tambwe kuchezewa faulo katika eneo la hatari.

Saimon Msuva bila ajizi aliiandikia yanga goli la kuongoza kupitia penati hiyo na kupelekea yanga kuongeza kasi na beki ya Kagera sugar kuonekana kuanza kukatika.

Dakika ya 14 Amisi Tambwe aliiandikia yanga goli la pili kabla ya Salum Kanoni kuifungia kagera sugali la kufutia machozi kwa mkwaju wa penati katika dakika ya 38.

Kipindi cha pili yanga waliendeleza kujilinda na kupeleka mashambuli ya kushtukiza huku Kagera wakizidi kulisakama lango la yanga kadri dakika zilivyokuwa zinasogea, hadi kipenga cha mwisho kinapulizwa yanga 2 Kagera sugar 1.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox