UONGOZI wa Klabu ya Simba umemtangaza Haji Sunday Manara kuwa ofisa habari mpya kwenye klabu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu Bara.
Katibu
Mkuu wa Simba, Stephene Ally alisema kuwa ofisa habari huyo ameteuliwa
na kamati ya utendaji baada ya kuona anakidhi vigezo.
Stephene
amesema, aliyekuwa ofisa wa timu hiyo, Humphrey Nyasio yeye
amebadilishiwa majukumu katika sekretarieti ya Simba katika kuhakikisha
wanafikia malengo yao.
“Uongozi
kwa jumla umelipitisha jina la Manara kuwa ofisa habari wetu katika
klabu yetu ya Simba na Nyasio aliyekuwa ofisa habari yetu
tumembadilishia majukumu mengine,” alisema Stephene.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni