KAMATI ya Utendajia ya Shirikisho la soka Tanzania (TFF) imepitisha ombi la usajili wa wachezaji saba wa kigeni kwa klabu za Ligi Kuu Tanzania Bara.
Hicho kilikuwa kilio kikubwa kwa klabu za ligi, hasa Yanga, Azam na Simba ambazo ndizo zinazosajili wachezaji wengi wa kigeni.
Kabla ya TFF kupitisha uamuzi huo, klabu ziliruhusiwa kusajili wachezaji watano wa kigeni bila kulipa TFF ada lakini sasa watalazimika kulipia kila mchezaji wa kigeni atakayesajiliwa.
Habari kutoka ndani ya kikao cha kamati ya utendaji kilichofanyika mjini Zanzibar leo, zilisema mvutano ulikuwa mkali wa ama kusajili wachezaji watano ama saba.
“Mjadala ulichukua muda mrefu sana, lakini kama unavyojua hiki kitu klabu kubwa zinamaslahi nacho, na ndio waliotoa ushawishi kwa wajumbe wengi kutaka usajili wa wachezaji saba mwisho tukakubaliana hivyo na hao saba wanaruhusiwa kucheza wote kwenye mechi moja,” alisema mtoa habari wetu kutoka ndaniya kikao hicho.
Lakini timu zimewekewa sharti gumu ambalo ni lazima kila mchezaji alipiwe ada ya dola za Marekani 2000 kwa mwaka lakini pia mchezaji anayesajiliwa kutoka nje lazima awe anacheza timu ya taifa ya nchi husika au Ligi Kuu.
Hii si mara ya kwanza kwa klabu za Ligi Kuu kuruhusiwa kusajili wachezaji zaidi ya watano, miaka ya nyuma ilikuwa ikisajili wachezaji kumi na kuruhusiwa kutumia watano kwenye mechi moja, lakini hakukuwa na masharti yoyote ya aina ya wachezaji wa kusajiliwa, hali iliyofanya klabu kusajili wachezaji wasio na uwezo, ama majeruhi ambao wakifika nchini hushindwa kutoa msaada kwa klabu husika.
Mwaka 2007 kulifanyika kangamano Bagamayo ambapo baadhi ya maazimio kwenye kongamano lile ni kupunguza idadi ya wachezaji wa kigeni ambapo ilikubalika mpaka msimu uliopita klabu zisajili wageni watano na watakaotumika kwa mechi moja wawe watatu.
Lakini hali imekuwa tofauti baada ya baadhi ya klabu kudai kuongezewa idadi ya usajili wa wachezaji wa kigeni ili zifanye vizuri kwenye michuano ya kimataifa.
TAREHE 20 JUNI, 2015 MAAMUZI YA KAMATI YA UTENDAJI Kamati ya Utendaji ya TFF imefanya kikao chake cha kawaida leo tarehe 20/06/2015 katika ukumbi wa Wizara ya Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo kisiwani Zanzibar, Baadhi ya maamuzi yake ni haya yafuatayo:
TUNZO ZA VODACOM. Baada ya kuzingatia mapungufu yaliyojitokeza katika uteuzi wa tuzo za ligi kuu ya Vodacom msimu wa 2014/15, Kamati ya utendaji imeagiza Rais wa TFF aunde kamati maalum ya kusimamia mchakato wa utoaji wa tuzo za Vodacom. Kamati hii itazingatia umuhimu wa kuhusisha idara za ufundi za TFF katika zoezi hilo na wadhamini na ligi watahusishwa kwa ukaribu katika zoezi hili.
KANUNI ZA LIGI 2015/16. Kamati ya utendaji ilipitia rasimu ya kanuni za ligi kuu, FDL na SDL za msimu ujao wa 2015/16. Mabadiliko makubwa yaliyofanywa ni kwenye maeneo yafuatayo:
LESENI ZA VILABU. Kamati ya utendaji imesisitiza kuwa hakuna klabu itakayopitishiwa usajili wake kama kupewa leseni ya klabu ya msimu.( Club Licencing).
WAAMUZI. Kamati ya utendaji imeridhia wazo la kamati ya maamuzi kuwa kuanzia msimu 2015/16 kutakuwa na jopo maalum ya waamuzi ( Elite referees) litakalochezeshwa mechi zote za ligi kuu. Waamuzi hawa watakuwa ni 16 wa kati, 32 wa pembeni na 4 wa akiba. Hii itasaidia kuongoza ufanisi katika uamuzi. (refereeing).
MGAWANYO WA MAPATO YA MILANGONI. Vilabu vimeongezwa mgawanyo wa mapato ya milangoni na sasa vitakuwa vinachukua asilimia 60% ya mapato ya mlangoni, makato mengine ni 18% VAT na 15% gharama za uwanja. UDHIBITI WA WACHEZAJI. Kanuni ilikuwa inatoa fursa timu ya kuamua mechi ipi mchezaji asicheze baada ya kuwa na kadi tatu za njano imefutwa.
KUSAJILI MIKATABA YA WACHEZAJI. Kuanzia sasa mikataba kati ya wachezaji na klabu itakayotambuliwa na TFF itakuwa ni ile ambayo ni nakala halisi zilizopigwa muhuri na lakiri ya TFF na kusajiliwa kwenye kumbukumbu ya TFF. Vilabu na mwachezaji watapewa nakala hizi baada ya kusajiliwa na TFF.
WACHEZAJI WA KIGENI. Kamati ya utendaji imeamua kuwa kuanzia msimu 2015/16 idadi ya wachezaji wa kigeni watakaosajiliwa na klabu ya ligi kuu itakuwa 7 (saba) wachezaji wote hawa, wote wataruhusiwa kucheza kwa wakati wote. Mikakati ya kusajiliwa wachezaji hawa ni haya yafuatayo: Mchezaji awe ni mchezaji wa timu za Taifa za nchi yake ( Senior, U23, U20, U19, U17 nk) au Mchezaji awe anacheza katika ligi kuu ya nchi yake au nchi nyingine wakati anasajiliwa. Kila mchezaji wa kigeni atakayesajiliwa atalipia ada ya maendeleo. Mpira wa vijana ya dola 2,000 kwa kila msimu atakyocheza hapa nchini. Fedha hizi zitapelekwa katika mfuko wa maendeleo ya mpira (Football Development Fund). Pia imeamriwa kuwa mikataba ya vilabu na wachezaji iliyo hai itaendelea kutambuliwa na TFF. Na kwa wale ambao tayari wapo nchini wataruhusiwa kuuhisha (to renew) mikataba yao iwapo watakubaliana na vilabu vyao.
4. LESENI ZA MAKOCHA Kamati ya utendaji imeamua kuwa kuanzia msimu huu, Kocha wa timu ya ligi kuu sharti awe na leseni B ya CAF au itakayolingana nayo kutoka katika mashirikisho mengine duniani na kocha msaidizi awe na leseni C ya CAF, hii ni kwa misimu mitatu. Kuanzia msimu wa 2018/2019 kocha wa Ligi Kuu atatakiwa kuwa na leseni A ya CAF au inayolingana na hiyo kutoka katika mashirikisho mengine duniani. Aidha Kamati ya Utendajji ya TFF imemteua Meshack Bandawe kuwa mjumbe wa bodi ya mfuko wa maendeleo ya mpira wa miguu - TFF (FDF), Bandawe ni meneja wa PPF kanda ya ziwa.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni