Licha
yakuahidiwa mamilioni ya shilingi, timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa
Stars’ imeshindwa kutamba nyumbani baada ya kuendeleza wimbi lake la
‘kunyolewa’ kufuatia kuangukia pua ka kichapo cha goli 2-0 kwenye mchezo
uliomalizika usiku huu kwenye dimba la Aman visiwani Zanzibar ikiwa ni
mchezo wa awali wa kutafuta kufuzu kushiriki mashindano ya Mataifa ya
Afrika kwa wachezaji wa ligi za ndani.
Mpira
ulianza wachezaji wa timu zote mbili kucheza mpira wa kubutuabutua
lakini baada ya dakika kadhaa mpira ulitulia na timu zote kuanza kupanga
mashambulizi. Lakini Stars bado wameendelea kuwa na matatizo yaleyale
ya kupoteza nafasi zinazopaikana kwa kukosa umakini pindi wanapokuwa
kwenye eneo la hatari la timu pinzani.
Kipindi
cha kwanza kilimalizika huku Uganda wakiwa mbele kwa goli 1-0
lililofungwa dakika ya 38 na Sekisambu baada safu ya ulinzi ya Stars
kutokuwa na umakini pamoja na golikipa Deogratius Munishi ‘Dida’ kuutema
mpira uliomkuta mfungaji na kuukwamisha wavuni kiurahisi kabisa.
Stars
ilipata nafasi kadhaa dakika za mapema lakini kutokana na kukosa
umakini kwa washambuliaji wa kikosi cha Stars nafasi zote
zilizotengenezwa ziliota mbawa. Beki wa kulia Shomari Kapombe alipiga
krosi mbili lakini zote ziliishia kwa walinzi wa Uganda. Lakini Amri
Kiemba, Abdi Banda na Simon Msuva walipata nafasi za kufunga lakini wote
walipoteza nafasi hizo.
Dakik
za mwanzo za kipindi cha pili Stars walianza vizuri kwani walicheza
mpira wa kasi na kuliandama lango la Uganda lakini bado mambo
yaliendelea kuwa magumu. Dakika ya 48 Salim Mbonde almanusura aipatie
Stars goli baada ya kuunganisha mpira wa kona uliogonga mtambaa panya na
kunyakwa na mlindamlango wa Uganda.
Dakika
ya 57 kocha wa Stars Mart Nooij alifnya mabadiliko kwa kumtoa Amri
Kiemba na nafasi yake ikachukuliwa na Said Ndemla….nz dakika ya 58 John
Bocco ‘Adebayor’ aliingia kuchukua nafasi ya Kelvin Friday.
Dakika
ya 63 mambo yaliendelea kuwa mabaya kwa Stars kwani Elisa Sekisambu
aliiandikia Uganda goli la pili ambalo lilionekana kumaliza kabisa
mipango ya Stars ambao walionekana wakicheza kila mtu kivyake na na sio
kitimu. Stars ikaanza kupoteza mipira ovyo na kupoteza umakini, Uganda
hawakufanya mashambulizi mengi lakini kila walipofika langoni mwa Stars
walikuwa ni mwiba ukilinganisha na mashambulizi yaliyofanywa na Stars.
Dakika
saba kabla ya pambano kumalizika, Nooij alimuingiza Rashid Mandawa
kuchukua nafasi ya Frank Domayo lakini mabadiliko hayo hayakuisaidia
chochote Stars kwani jahazi lake bado liliendelea kuzama.
Dakika
ya 88 ndipo ndoto za Tanzania ziliota mbawa baada ya Stars kutandikwa
goli la tatu lililofungwa kwa mkwaju wa penati na kufuatia Nadir Haroub
‘Cannavaro’ kumwangusha mchezaji wa Uganda kwenye eneo la hatari. Farouk
Meya aliifungia Uganda penati iliyowahakikishia ‘The Cranes’ ushindi wa
ugenini.
Stars
itakuwa na kibarua kigumu kwenye mchezo wa marudiano utakaopigwa kwenye
uwanja wa Namboole jijini Kampala, Uganda wiki mbili zijazo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni