STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumatatu, 20 Aprili 2015

ETOILE DU SAHEL WAKATA MZIZI WA FITINA KUHUSIANA NA OKWI


Okwi enzi hizo akiwa Etoile.
Wakati wewe ulifikiri Etoile du Sahel wana mpango wa kulipa zile dola 300,000 (Sh milioni 480), wenyewe walikuwa jijini Dar es Salaam wakisaidiana na Shirikisho la Soka la Tunisia (FTF) wakitaka kumpata Emmanuel Okwi.

Makamu wa Rais wa FTF, Krifa Jalel, amesema walimsaka Okwi bila mafanikio ili wazungumze naye na kujua sababu ya kutoroka kazini.




Jalel amesema waliomba waletewe Okwi bila ya mafanikio na walishirikiana na Rais wa Etoile du Sahel (ESS), Charefeddine Ridha aliyekuwa jijini Dar es Salaam kumpata Okwi.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, juzi, Jalel alisema anashangazwa na kuona Simba wanadai fedha wakati Okwi sasa anaichezea Simba.

“Sasa wanataka walipwe fedha za nini? Okwi si yuko hapa anaichezea Simba? Tumetaka kukutana naye ili tuzungumze na kutatua tatizo lake, hakuna aliyetusaidia kumpata.

“Nilizungumza na baadhi ya viongozi wamlete, hakuna aliyetusaidia. Nilitaka kumuuliza kwa nini aliondoka Tunisia baada ya miezi sita na hakurejea,” alisema na alipoulizwa kama ni viongozi wa Simba ambao hawakuwapa msaada alisisitiza:

“Wewe jua ni viongozi tena wahusika. Sasa sioni kama kuna sababu ya kulipa ingawa bado Etoile ndiyo watalitolea uamuzi.”

Alipofuatwa kiongozi mwingine wa Etoile, yeye alisema suala la Okwi liliisha na hawana sababu ya kulizungumzia kwa kuwa yupo Dar es Salaam walipomtoa na anaichezea timu yake ya zamani, hivyo hakuna kilichoharibika.

“Nafikiri unataka kunitega sijui niseme nini. Okwi yupo hapa kwenu anaichezea timu yake. Sasa tulipe kwa kuwa anaichezea Simba! Si tayari Simba wana mchezaji wao,” alihoji.

Etoile iliahidi kulipa fedha hizo kwa ajili ya Okwi baada ya Simba kukubali kumuuza ‘bure’ kupitia aliyekuwa mwenyekiti wake, Ismail Aden Rage.

Lakini Simba imesema tayari Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), limeagiza Simba ilipwe fedha hizo lakini Etoile wamekuwa wakisuasua na kauli walizozitoa katika mahojiano hayo juzi, zinaonyesha huenda fedha hizo kulipwa, itakuwa ndoto kama Simba wasiposimama kidete.

SOURCE: CHAMPIONI

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox