STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumatano, 1 Aprili 2015

HARRY KANE ANA THAMANI YA PAUNI MILIONI 100, UBORA NI ZAIDI YA DI MARIA!


Harry Kane ana thamani ya Pauni Milioni 100 kwa mujibu wa Straika wa zamani wa England Rodney Marsh.
Kinda huyo wa Miaka 21 ameibuka Msimu huu na kuifungia Klabu yake Tottenham Mabao 29 na Ijumaa iliyopita, akiichezea England kwa mara ya kwanza kabisa, alifunga Bao lake la kwanza Sekunde 79 tu tangu aingizwe kutoka Benchi.

Rodney Marsh, ambae aliichezea England mara 9, amesema: "Thamani yake sasa ni Pauni Milioni 100. Nadhani atapanda na kuwa bora kupita Alan Shearer,Man City ililipa Pauni Milioni 32 kumnunua Mchezaji asiejulikana Eliaquim Mangala. Ikiwa Mangala thamani yake ni Pauni Milioni 32, Harry Kane ni lazima thamani yake ni Pauni Milioni 100!"
Aliongeza: "Angel Di Maria ameigharimu Man United Pauni Milioni 60. Nadhani Harry Kane ni Mchezaji bora kupita Di Maria!"

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox