Sepp
Blatter amesisitiza kuwa ana uwezo mkubwa wa kuifanya Fifa iwe safi na
kuirudishia heshima yake ya awali baada ya kuchaguliwa tena kuliongoza
shirikisho hilo kubwa linalosimamia kandanda ulimwenguni.
"Ningependa
kutoa shukrani zangu za dhati kabisa kwa Prince Ali kwa sababu ni
mshindani, mpiganaji na amepata matokeo mazuri tu," Blatter mwenye umri
wa miaka 79 alisema katika hotuba yake baada ya ushindi wake.
"Kwa upande mwingine , nawashukuru wanachama wa Fifa kwa kunichagua kulitumikia shirikisho hili kwa miaka mingine minne.
"Nitakuwa
ni muongozaji wa boti hili linalojulikana kwa jina la Fifa na
kulifikisha mahali panapohusika ili tuwezeshe kuufukissha mpira wetu
mahali pake, lakini tunatakiwa kufanya kazi kweli kweli.
"Mnakumbuka
miaka minne iliyopita baada ya kuchaguliwa kuongoza tena Shirikisho
hili, nilikuwa na mambo mengi sana ya kuyatatua. Niliwapa changamoto
kipindi kile, Lakini safari hii sitafanya hivyo ila tunatakiwa kuyatatua
baadhi ya matatizo yanayoyakabili baadhi ya mashirikisho ili tuweze
kufanya kazi kwa uhakika zaidi,"alisema Blatter.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni